Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora
akifurahia kazi nzuri inayofanywa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali
alipofanya ziara fupi kiwandani hapo jijini Dar es Salaam tarehe 20
Februari 2018.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora
akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Kaimu Mpiga Chapa Mkuu wa
Serika alipotembelea kiwanda hicho na kukutana na wafanyakazi jijini Dar
es Salaam tarehe 20 Februari 2018.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora
akiongea na wafanyakazi wa kiwanda cha Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali,
(katikati) Kaimu Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. John Kaswalala, jijini Dar es Salaam tarehe 20 Februari 2018.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora
awataka watumishi wa ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kujituma na wawe wabunifu ili kuzalisha kwa ufanisi zaidi.
Amesema hayo alipotembelea kiwanda cha Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kilichopo jijini Dar es salaam,tarehe 20 Februari 2018.
Amewasisitiza
wafanyekazi kwa nguvu, wajue vifaa wanavyotumia na kuvielewa ili kuweza
kufanya kazi kwa urahisi na kuepuka uharibifu wa mashine hizo, watambue
kuwa Serikali inazidi kuboresha mazingira ya kazi na taratibu za
kuendesha shuguli zake za kiuchumi.
“Tunaishi
katika ulimwengu wa maarifa,hivyo maarifa tuyatumie kazini kwa kuwa
wabunifu na kufahamu vizuri mitambo na vifaa tunavyotumia ili tuweze
kuzalisha kwa ufanisi ili wote tufaidike na matunda ya uzalishaji huo.”
Alisema Prof. Kamuzora.
Akielezea
juu ya uendeshaji shughuli za kiwanda hicho Kaimu Mpiga Chapa Mkuu wa
Serikali Bw. John Kaswalala alisema, kiwanda hicho kinaendelea kukua
kiuchumi na kuimarika. Aidha, watumishi wa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali
wamempongeza sana Prof. Kamuzora kwa utendaji wake na kufika kwake
katika ofisi zao, na kuomba serikali izidi kuwawezesha kwa vifaa,
mitambo na teknolojia ili wazidi kuzalisha zaidi.
Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu
Dar es Salaam, 21 Februari, 2018
0 comments:
Post a Comment