Usajili upo wazi kwa watumiaji wote wa mtandao wa Tigo
Tigo Kili Half Marathon kuhamasisha afya bora miongoni mwa Watanzania
21 Januari, 2018. Dar es Salaam. Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania leo imetangaza kuanza kwa usajili wa mbio ndefu za Tigo Tigo Kili Half Marathon kupitia namba *149*20#.
Kwa mwaka wa nne mfululizo, Tigo ndio mdhamini mkuu wa mbio za KM 21 za Tigo Kili Half Marathon ambazo zitafanyika tarehe 4 Machi mwaka huu, katika viwanja vya Ushirika, mjini Moshi. Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa shindano la Tigo Kili Half Marathon 2018 linaunga mkono juhudi za serikali za kuinua viwango vya michezo na kujenga afya bora za Watanzania kupitia ushiriki wao katika michezo.
“Usajili wa mbio za Tigo Kili Half Marathon pamoja na mbio nyingine za KM 5 na KM 42 upo wazi kwa watumiaji wote wa mtandao wa Tigo kupitia namba *149*20#. Kujisajili, piga simu namba *149*20#, kisha fuata maelekezo rahisi ya kuchagua mbio unazotaka kukimbia na kulipia ada ya usajili kwa mbio husika. Baada ya kutuma ada ya ushiriki, utapokea ujumbe mfupi wa maneno (SMS) utakaokujulisha kuhusu kukamilika kwa muamala wako. Utunze ujumbe huu mfupi wa maneno na kisha nenda nao pamoja na kitambulisho chako halisi katika kituo utakachojulishwa katika miji ya Dar es Salaam, Arusha na Moshi ili kuchukua namba yako ya ushiriki,’ Woinde alieleza.
Tigo inatoa jumla ya TZS 11m kama zawadi kwa washindi kumi wa kwanza wa mbio za Tigo Kili Half Marathon kwa upande wa wanaume na wanawake. Pia kuna medali na vyeti vya ushiriki kwa watu 4,500 wa kwanza watakaomaliza mbio hizo.
‘Tunachukua fursa hii kuwakaribisha washiriki wote, ikiwemo wanariadha wa kimataifa, wa kitaifa, wapenda michezo na wanafamilia wote kuja kushiriki katika mbio hizi za Tigo Kili Half Marathon, ili waweze kutunza afya zao pamoja na kufurahia kumbukumbu za matukio yanayoendana na shamrashamra za mashindano,’ Woinde alisema.
Naye Afisa wa Lipa Kwa Tigo Pesa, David Chinguile alisema kuwa Tigo imepanua huduma ya Tigo 4G kufikia miji 22 nchini Tanzania, ikiwemo katika mji wa Moshi na kanda yote ya Kaskazini. Uwekezaji huu mkubwa utahakikisha kuwa watakaohudhuria Tigo Kili Half Marathon 2018 watapata huduma bora na za uhakika za mtandao wa simu utakaowawezesha kuwasiliana na ndugu, jamaa, na marafiki pamoja na kutuma picha na video za matukio na kumbukumbu nyingine muhimu kwa kasi ya juu kupitia mtandao wa Tigo 4G.
Tigo inajivunia kuwa sehemu ya mbio za Tigo Kili Half Marathon 2018 ambazo zinazidi kujizolea umaarufu mkubwa ulimwenguni mwaka hadi mwaka.
0 comments:
Post a Comment