Wanawake wametakiwa kuzingatia uvaaji wa viatu vyenye kisigino kifupi kuimarisha afya ya miguu na kuepuka kuvaa viatu vyenye kisigino kirefu ama kisigino flati ambavyo ni hatari kwa afya ya magoti.
Akizungumza na wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD) kanda ya Mabibo katika kambi ya matibabu ya siku mbili ya uchunguzi wa afya Mtaalamu wa mazoezi tiba kutoka JKCI Jaqline Mariki alisema mtu anatakiwa kuvaa viatu vyenye kisigino kifupi ili unyayo uweze kunyanyuka kidogo kusaidia ugawanyishwaji wa uzito kwenye mwili hivyo kutoleta maumivu katika mwili.

0 comments:
Post a Comment