Katika kuelekea kilele cha Malkia wa Nguvu 2025 inayoratibiwa na Chombo cha Clouds.
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umewafikia Malkia na Balkia katika Soko la Kariakoo, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa elimu, kuandikisha wanachama wapya waliojiajiri ili waweze kujiunga na kujiwekea akiba kwa kuchangia shilingi 30,000 au zaidi kwa kutoa kidogo kidogo kwa siku bukubuku, wiki, mwezi au msimu kulingana na kipato chake na hapo baadae wote watakuwa wanufaika ws mafao yote yanayotolewa na NSSF yakiwemo ya uzee, uzazi na matibabu.
Akizungumza katika kipindi cha Leo Tena kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha Clouds Fm, Bw. Shabani Mbwana, Afisa Matelekezo Mkuu wa NSSF, amesema lengo la kuanzishwa kwa Mfuko ni kuhakikisha wananchi wanapata kinga dhidi ya majanga kama uzee au kupungua kwa kipato ambapo mtu anayejiwekea akiba anapopatwa na majanga ya aina hiyo atanufaika na mafao kutoka NSSF. Aidha, amesema kuwa Mfuko umeanzisha Skimu maalumu kwa ajili ya wananchi waliojiajiri hivyo amewataka kujiunga na kuchangia ili wawe Mastaa wa Mchezo pale watakaposhindwa kufanya kazi za uzalishaji mali waweze kunufaika na mafao na huduma nyingine zinazotolewa NSSF.
0 comments:
Post a Comment