Home » » *MSONDO NGOMA YATOA RATIBA YA KUWASHA MOTO SIKUKUU YA PASAKA

*MSONDO NGOMA YATOA RATIBA YA KUWASHA MOTO SIKUKUU YA PASAKA



BENDI kongwe ya muziki wa dansi Tanzania, Msondo Ngoma ‘Baba ya Muziki’ imetoa ratiba ya maonyesho yao katika kusherekea Sikukuu ya Pasaka ambapo wataanza kutoa burudani ndani ya ukumbi wa Wipes Bar Mivinjeni Kurasini na siku ya Ijumaa watakuwa Leanders Club Kinondoni, Jumamosi watakuwa TCC Club Chang’ombe, Pasaka watakuwa Kata ya 14 Temeke na
Jumatatu ya Pasaka watakuwa sambamba na FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.

Akizungumza na mtandao huu wa www. sufianimafoto.blogspot.com, msemaji wa bendi hiyo,  Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa wameamua kutoa ratiba hiyo ili mashabiki wao waweze kujua nini kinachoendelea ndani ya bendi yao na waweze kujipanga ili kupata burudani ya sikukuu ya Pasaka..

Aidha alisema kuwa hata hivyo tayari wamajipanga vizuri katika suala zima la kutoa burudani ya kukonga nyoyo za mashabiki wao katika kusherekea sikukuu hii ya Pasaka.

Hata hivyo aliongeza kuwa wanahitaji mashabiki wao kjitokeza kwa wingi ili waone nini wanachowapa katika siku hizo zote kwani sikukuu ya pasaka ni muhimu kusherekea na msondo ngoma bendi hiyo inayotamba na vibao vyake vipya vya Suluhu wa Shabani Dede na Nadhiri ya Mapenzi wa Juma Katundu pia watapiga nyimbo zao zote zilizotamba kipindi cha nyuma alisema Super D

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa