na Asha Bani
NAIBU
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema hali ya ujangili kwa
sasa ni mbaya nchini na kwamba kunahitaji nguvu za ziada kupambana nao.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu kukamilika kwa
maandalizi ya kongamano la kwanza la Afrika litakalofanyika Oktoba 15 hadi 18,
alisema pia ujangili upo hata katika nchi za Afrika Mashariki ambazo
zimeizunguka Tanzania.
Alisema
hali hiyo imechangiwa na nchi za Japan, Marekani, Taiwan kutokana na kuwapo kwa
uhitaji mkubwa wa rasilimali zitokanazo na wanyama.
Hata
hivyo, alisema serikali itaongeza nguvu katika kuhakikisha kuna ulinzi wa
kutosha katika mbuga sambamba na silaha pamoja na askari.
Akizungumzia
maandalizi ya kongamano hilo lililoandaliwa na Shirikia la Umoja wa Mataifa la
Utalii Duniani (UNWTO) ambapo Tanzania wamechaguliwa kuwa wenyeji, alisema
yamefikia hatua ya mwisho na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais,
Mohamed Ghalib Bilal .
Alisema
katika mkutano huo watu 412 kutoka katika nchi 40 za Afrika wamejisajili kushiriki.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment