na
Happiness Katabazi
SIKU
moja baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kuwahukumu adhabu ya kifo
askari wa wiwili wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mmoja wa Jeshi la Wananchi
(JWTZ) kwa kosa la kumuua kwa kukusudia Swetu Fundikira, wafungwa hao jana
wamewasilisha hati mahakamani hapo ya kusudio la kukata rufaa kupinga hukumu
hiyo.
Wafungwa
hao ni MT 1900 Sajenti Roda Robert (42), MT 85067 Koplo Mohamed Rashid wa
JKT Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa kikosi cha JWTZ Kunduchi.
Wakili
wa askari wa wafungwa hao, Mluge Karoli, alisema ameishawasilisha hati hiyo
mahakamani hapo jana kwa madai kuwa wateja wake hawakubaliani na hukumu hiyo
iliyotolewa juzi na Jaji Zainabu Mruke ambaye aliwatia hatiani kwa kosa la kuua
kwa kukusudia kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya
mwaka 2002.
Karoli
alieleza kuwa sababu zilizomsukuma yeye na wateja wake kuwasilisha hati hiyo ni
kwamba kesi yoyote ya ugomvi haiwezi kuwa na kusudio la
kutaka kuua na kwamba hakuna shahidi wa upande wa jamhuri aliyefika mahakamani
hapo na kueleza kuwa wateja wake ndiyo wamemuua Swetu Fundikira.
Alieleza
kuwa, aliyepambana na wateja wake ni Swetu Fundikira na uchunguzi wa daktari
unaonyesha jina la Swetu Ramadhani Fundikira hivyo ni watu wawili tofauti, na
kwamba hakuna hata shahidi mmoja alifika mahakamani na kueleza aliwahi
kuuona mwili wa marehemu au kuhudhuria kwenye msiba.
Askari
hao kwa pamoja walidaiwa kuwa walimpiga Fundikira, Januari 23 mwaka huu saa
7:30 usiku wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam na baadaye kufariki dunia
usiku huo huo wa kuamkia Januari 24, mwaka 2010, katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili.
Akisoma
hukumu hiyo juzi , Jaji Muruke alisema ingawa hakuna ushahidi wa moja kwa moja
kuwa washtakiwa hao ndio waliomuua Fundikira, ushahidi uliotolewa na
upande wa mashtaka (Jamhuri) ulikuwa ni ushahidi wa mazingira, kwamba Jamhuri
imeweza kuthibitisha mashtaka hayo.
CHANZO MTANZANIA DAIMA
0 comments:
Post a Comment