AY amesema kampuni yake ya Unity Entertainment haimsimamii tena aliyekuwa mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa The Chase, Feza Kessy.
AY amekiambia kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen jana kuwa hajawahi kukutana na Feza tangu arejee kutoka kwenye shindano hilo.
“Tangu ameenda Big Brother na akarudi hatujawahi kukutana face to face,” alisema AY.
“Kulikuwa na vitu kidogo ambavyo viko nje ya kikawaida kama unafanya kazi na artist vinatakiwa vifanyike. Kwahiyo tukaona labda alikuwa anatafuta tu opportunity fulani ya kukamilisha mambo fulani. Katika policy zetu za kampuni ni kuwa hatufanyi kazi kwa njia hiyo, kwahiyo tuliamua kumweka pembeni.”
AY amesema tayari alishaongea na Feza na kumtakia kila lakheri kwenye kila jambo atakalolifanya.
“Hata yeye mwenyewe tu nilimwambia namtakia kila lakheri, cha msingi atumie hiyo opportunity aliyoipata sasa hivi ili kufanya mambo mengine kama washiriki wengine wanavyoenda katika Big Brother.”CHANZO BONGO5
0 comments:
Post a Comment