Mery
Kanyaga, akimpongeza binti yake, Shelder Boniface ambaye ni
mshambuliaji wa timu ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 ‘The
Tanzanite’ muda mfupi baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo, wakitokea Msumbiji
katika mechi ya marudiano ya kufuzu fainali za Dunia za wanawake ambako
Tanzanite iliichapa Msumbiji mabao 5-1 huku Shelda akitupia matatu kati
ya hayo.
Mery Kanyaga, akiwa amepozi na binti yake, Shelder Boniface mara baada ya kuwasili akitokea Msumbiji na timu ya taifa ya wanawake ya Tanzanite. Shelder aliifungia timu yake mabao matatu.
Nahodha wa The Tanzanite, Fatuma Issa akizungumza na waandishi wa habari.
Baadhi ya wazazi wakiwa na watoto wao baada ya kuwasili jijini Dar es Salam wakitokea Msumbiji.

Baadhi ya wachezaji wa timu
ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 ‘The Tanzanite’
wakipanda basi baada ya kuwasili leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wakitokea Msumbiji.
Wachezaji
The Tanzanite wakiwapungia mikono mashabi waliofika kuwapokea kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
jana, wakitokea Msumbiji.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura
akipeana mkono na wachezaji wa Tanzanite mara baada ya timu hiyo
kuwasili jijini Dar es Salaam ikitokea Msumbiji.
Wachezaji
wa timu ya taifa ya wananwake chini ya umri wa miaka 20 'Tanzanite'
wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea Msumbiji katika mchezo wa
kufuzu fainali za kombe la Dunia la wanawake dhidi ya Msumbiji, ambako
Tanzania ilishinda 5-1.
Baadhi ya wachezaji wa timu
ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 ‘The Tanzanite’
wakiwasili leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam, wakitokea Msumbiji katika mechi ya marudiano ya
kufuzu fainali za Dunia za wanawake ambako Tanzanite iliichapa Msumbiji
mabao 5-1. Picha zote na Francis Dande
Picha ya kwa hisani ya Michuzi
0 comments:
Post a Comment