Home »
» Apeneta yatakiwa kuwajengea uwezo wajasiriamali
Apeneta yatakiwa kuwajengea uwezo wajasiriamali
ASASI
ya kiraiaya inayojishughulisha na ukuzaji wa uchumi nchini (APENETA)
ambayo imetakiwa kuwajengea uwezo wa uthubutu wajasiriamali ili waweze
kujikomboa na umaskini.
Hayo yalisemwa juzi na ofisa miradi wa
taasisi ya Tanzania Aid Development (TZAD) Hamis Tembo ambaye
alimwakilisha Dismas Liyasa wakati akizindua mfuko wa kikundi cha
Wazalendo cha mtaa wa Mongolandege kata ya Ukonga ambapo TZAD waliahidi
sh.500, 000.Alisema kuwa wajasiriamali wengi wanashindwa kufikia malengo
yao kwa kuwa hawajengewi uwezo wa kujiamini na kuthubutu wakati wa
kuendesha biashara zao .
Wakati huo huo, Diwani wa Kata ya Ukonga
Elizabeth Mbano ameziomba Halmashauri nchini kuhakikisha wanatumia Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ili kuwaletea tija jamii.
" Lengo kuu
la mfuko huu ni kusimamia na kuiletea jamii maendeleo hivyo ni jambo
ambalo kwa upande wa Halmashauri wamejipanga kuhakikisha hayo
yanatekelezeka kwa asilimia 100," alisema.
Hata hivyo, mkurugenzi wa
asasi ya Apeneta Gration Mutoshbya amesisitiza kutumia fursa mbalimbali
wanazozipata ili wajasiriamali wawe na uelewa sahihi juu ya kupiga vita
umaskini.
Naye Katibu wa asasi hiyo Christopher Pigangoma ameiomba
Serikali kupitia wadau wake ili kuipa fedha asasi hiyo iweze kuzitumia
kusomesha watoto yatima na makundi mengine maalumu kwa ajili ya
kuipunguzia taifa mzingo mkubwa.
Aidha kwa upande wake mwezeshaji wa
kikundi cha Wazalendo Nasra Athumani amewataka Watanzania kuendeleza na
kuthamini rasilimali zilizopo kwa lengo la kusaidia jamii iliyopo na
kukuza uchumi.
Chanzo;Majina
0 comments:
Post a Comment