Home » » Wabunge wataka Takukuru kuweka dawati Hazina

Wabunge wataka Takukuru kuweka dawati Hazina

William Ngeleja
 
Kamati  ya Bunge ya Kudumu ya Katiba, Sheria na Utawala, imeishauri serikali kuangalia uwezekano wa kuwa na dawati maalumu la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) katika ofisi ya Kamshna wa Bajeti katika Wizara ya Fedha.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, William Ngeleja, alisema jijini Dar es Salaam jana, mara baada ya Kamati yake kutembelea Takukuru na kupata maoni yao katika kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma kwenye miradi ya maendeleo.

Alisema kamati hiyo itashirikiana na kamati za kisekta kuishawishi serikali kuwa na dawati litakalokuwa na ofisa wa Takukuru ambaye kazi yake itakuwa ni kuangalia jinsi fedha za miradi ya maendeleo zinavyotoka na kuelekezwa katika maeneo mbalimbali kwa kuwasiliana na maafisa wake walioko mikoani.

“Hakuna ubishi kuwa asilimia 60 hadi 70 ya bajeti ya nchi inaelekwezwa kwenye Halmashauri na huko ndiko kuna uchakachuaji wa fedha za miradi ya umma, thamani ya fedha haipo, tukiwa na Ofisa wa Takukuru wizarani atafuatilia kwa karibu na kujua mrija unaovujisha fedha hizo uko wapi,” alisisistiza.

Ngeleja alisema Takukuru ilipendekeza kupewa nguvu ya kufuatilia matumizi ya fedha za miradi kwenye miradi mbalimbali, lakini kamati iliona muundo huo hautatibu tatizo kwa kuwa utakuwa unashughulika na matawi na kuacha mizizi.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa