Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (kulia)
akikata utepe kuzindua ripoti ya hali ya Uwekezaji nchini Tanzania leo
jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine ripoti hiyo imegusia sera
na na maendeleo ya uwekezaji nchini pamoja na changamoto zinazokwamisha
ustawi wa uwekezaji Tanzania.
Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda akionyesha vitabu vya ripoti ya Uwekezaji
Tanzania kwa wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa ripoti kuhusu
hali ya Uwekezaji nchini Tanzania leo jijini Dar es salaam.
Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi kitabu cha Ripoti ya hali Uwekezaji
nchini Tanzania Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dkt. Reginald Mengi (kulia)
leo jijini Dar es salaam.
Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na wadau wa uwekezaji mara baada ya
kuzindua ripoti kuhusu hali ya uwekezaji nchini Tanzania.
Mwenyekiti
Mtendaji wa IPP Dkt. Reginald Mengi (kulia) akizungumza jambo na Bi.
Marry Hobbs Mwakilishi wa masuala ya Kilimo na Maliasili wa Shirika la
Misaada la Watu wa Marekani nchini Tanzania leo wakati wa Uzinduzi wa
ripoti ya hali ya Uwekezaji nchini.
Wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa ripoti ya Uwekezaji nchini Tanzania leo jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Titus Kamani akitoa ufafanuzi kwa
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu changamoto na hali
ya uwekezaji katika sekta ya Mifugo na uvuvi nchini.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
0 comments:
Post a Comment