Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza.
Akitoa uwamuzi huo, Chiza alisema amefikia maamuzi hayo baada ya kupitia ripoti ya timualiyoiunda kwa lengo la kubaini chanzo cha mgogoro huo wa muda mrefu.
“Nimepitia kwa makini taarifa ya kamati niliyoiunda kunisaidi kufanya uchunguzi wa kina juu ya rufaa iliyokatwa kwangu na Amiri Mrisho Mbanga na wezake 77 dhidi ya uamuzi uliotolewa awali kuhusu madai ya warufani kukataliwa kuwa siyo wanachama wa DASICO LTD,” alisema Chiza.
Aliongeza: “Baada ya kujiridhisha na ripoti ya kamati na kwa mamlaka niliyopewa chini ya kanuni ya 52(6) ya kanuni za ushirika 2004 natoa maamuzi ya kuwarudisha katika ushirika Amiri Mbanga, Abdallah Mkumba, Ramadhan Ndile, Ally Kiumulio, Mohammed Fungo, Sadiki Mpale, Hmisi Mbwana, Mwana Muhua, Said Lupemba, Haidary Mvugalo na Hamisi Simbaulanga kuwa niwanachama halali wa DASICO kwakuwa walitimiza masharti ya kulipa kiingilio.”
Hata hivyo, Chiza alisema wanachama wengine ambao walisimamishwa watakapothibitisha kuwa walilipa viingilio na kuonyesha risiti zao watarudishiwa uanachama wao.
Mgogoro wa wanachama hao ulichukua zaidi ya miaka 20 tangu mwaka 1993 baada ya walalamikaji kwenda mahakamani na kuagizwa wapeleke shauri lao kwa mrajis kama sheria ya vyama vya ushirika inavyosema.
Mbanga kwa niaba ya wenzake, alisema alisema anashukuru maamuzi ya Waziri Chiza ambaye ametambua haki ya wanyonge.
Akizungumzia hukumu hiyo, Mrajis Mkuu, Dk. Audax Rutabanzibwa, alisema vyama vya ushirika vinatakiwa vichague viongozi wenye weledi ili kuepusha migogoro ya mara kwa mara ambayo inarudisha nyuma maendeleo ushirika.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment