Home » » DAKTARI FEKI AKAMATWA MUHIMBILI TOA MAONI JINA NA MAHALI

DAKTARI FEKI AKAMATWA MUHIMBILI TOA MAONI JINA NA MAHALI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Hospitali ya taifa ya Muhimbili imemkamata mtu mmoja anae sadikiwa kuwa daktari feki ambaye kwa kipindi cha kirefu amekuwa akitapeli wagonjwa wanaoenda kutibiwa katika hospitali hiyo ya taifa kwa namna mbalimbali
Daktari huyo aliyejulikana kwa jina la Kitano Mustafa Kitani mwenye umri miaka 51 anadaiwa kuwa alikuwa anajitambulisha kama daktari upande wa akina mama katika hospitali ya Muhimbili.
Hospitali ya taifa ya Muhimbili mbali na utaratibu wa kutumia vitambulisho kwa wafanyakazi ili kuondoa tatizo kama hili, bado tatizo hili limeendelea kujitokeza.
Hospitali ya Muhimbili inawataka wafanyakazi wake wanaoshirikiana na madaktari vishoka kuacha tabia hiyo yenye athari kwa wagonjwa na taifa.
Chama cha Madaktari nchini kimewataka wananchi kuwa na macho na madaktari wanaotokeza kutaka kusaidia wagonjwa.
Wakati daktari huyo akidai yeye ni daktari kitaaluma, Afisa Usalama hakubaliani nae kutokana na taarifa za kiuchunguzi zinazothibitisha kuwa ni feki.
Hili ni tukio la tatu kutokea katika hospitali ya Muhimbili.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa