Home » » Gesi asili yawavutia wawekezaji wa Misri

Gesi asili yawavutia wawekezaji wa Misri

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Wawekezaji mbalimbali wa Misri wameonyesha nia kuwekeza Tanzania zaidi ya dola 5 milioni za Marekani, hasa eneo la gesi asilia na huduma nyingine.
Msemaji wa Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Badr Abdelatty alisema Dar es Salaam juzi kuwa, wawekezaji wa Misri wanataka kuwekeza zaidi sekta ya nishati hasa gesi.
“Tunakubali kuwa Misri kwa sasa imechafuka, hali ya kisiasa siyo ya kuridhisha, lakini haituzuii kuja kuwekeza. Tunataka kuwekeza Tanzania,” alisema Abdelatty.
Alisema kuwa mpango wao si kutoa huduma za kiufundi lakini zaidi ni kuendeleza sekta ya,
kilimo, usafiri wa reli na barabara, nishati, mawasiliano, umwagiliaji na ujenzi wa viwanda vya
kuzalisha saruji.
“Si Tanzania pekee iliyopangwa kwa ajili ya uwekezaji, tunaangalia uwezekano wa kuendeleza
kazi hiyo kwa mataifa mbalimbali ya Afrika.”
Hata hivyo, alisema kuwa ushirikiano wa Tanzania na Misri ulianza siku nyingi kwani Misri ina
mpango wa uboreshaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili huku ikisomesha
zaidi ya wanafunzi 300 wa Tanzania katika vyuo vikuu mbalimbali nchini Misri.
Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Misri, Akmal Zaghloul alisema kuwa kuimarika
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa