Tunakuletea matukio ya moja kwa moja kutoka kwenye Mkutano Mkuu wa tatu wa wadau utakaofanyika leo tarehe 26 na kesho 27 Februari 2014 kuanzia katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Madhumuni ya Mkutano huu ni kutoa taarifa ya hesabu ya mwaka na utendaji wa Mfuko na kutathmini mafanikio na changamoto zinazokabili Mfuko na sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa ujumla.
Mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Hassan Mwinyi, kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, kulia kwake ni Ndugu Peter Ilomo aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF George Yembesi, Mkurugenzi Mkuu PSPF, Adam Mayingu na Katibu Mkuu MPAIC, John Haule
Matukio zaidi kutoka kwenye mkutano huu yatakujio hapa endelea kuwa nasi.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment