Askari
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakibeba mwili wa marehemu Meja
Mstaafu Samwel Isaac Chekingo mara baada ya kuwasili nyumbani kwake
Kinondoni kwa ajili ya ibada maalum.
Marafiki
wa karibu wa familia ya marehemu wakiwa wamesimama kuupoke mwili wa
marehemu Meja Mstaafu Isaac Chekingo ulipowasili nyumbani kwake
Kinondoni jijini Dar mwishoni mwa Juma.
Mtoto
mkubwa wa marehemu (mwenye koti la suti jeusi) akijadiliana jambo na
baadhi ya wanakamati wa msiba ulioongozwa na Afande Thomas Ndonde wa
JWTZ.
Baadhi ya waombolezaji wakitoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu Meja Mstaafu Samwel Isaac Chekingo.
Baadhi ya watoto wa marehemu na wake zao wakiwa kwenye majonzi mazito.
Mtoto
mkubwa wa marehemu Samson Samwel Chekingo (mwenye miwani) akijadiliana
jambo na wadogo zake kabla kuanza kwa misa ya kumwombea marehemu baba
yao.
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Meja Mstaafu Samwel Isaac Chekingo mara baada ya kuwasili nyumbani kwake.
Aliyewahi
kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Lawrence Masha (katikati) akiwa
amejumuika na baadhi ya waombolezaji kwenye msiba wa Marehemu Meja
Mstaafu Samwel Chekingo.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamefurika nyumbani kwa marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo.
Mchungaji
Charles Mzinga kutoka Kanisa la Usharika wa Azania Front akiendesha
ibada ya misa ya kumwombea marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo
iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Kinondoni jijini Dar mwishoni mwa
juma.
Aliyewahi
kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Lawrence Masha akijumuika na
waombolezaji wengine kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Meja Mstaafu
Samwel Chekingo.
Waombolezaji wakiendelea kutoa heshima za mwisho.
Pichani
juu na chini ni watoto wa marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo wakitoa
heshima za mwisho kabla ya kuelekea makaburi ya Kinondoni kwa ajili ya
mazishi.
Vilio na simanzi vilitawala.
Mke wa marehemu akitoa heshima za mwisho kwa mpendwa mume wake.
Pichani juu na chini Familia ya marehemu ikiwa katika makaburi ya Kinondoni tayari kuanza shughuli za mazishi.
Kwa picha zaidi ingia humu
WASIFU WA MAREHEMU MEJA SAMUEL ISAAC CHEKINGO.
Marehemu alizaliwa tarehe 06.06.1953, alizaliwa Ng’ang’ange, Dabaga na alikulia Mufindi kibaoni – Mgelukwa.
Alisoma shule ya msingi Mufindi na shule ya sekondari Kigonsela.
Baada
ya hapo alijiunga na Jeshi la Ulinzi wa Tanzania, na alihudhuria kozi
mbalimbali za kijeshi, zaujuzi na uongozi. Pia kozi na kozi ya taaluma
ya urubani nchini Canada.
Marehemu alitunukiwa medali mbalimbali za kijeshi zikiwemo:-
a) Medali za Ushindi.
b) MedaliVita ya Kagera.
c) Medali ya Miaka Miaka Ishirini ya Utumishi.
d) Utumishi wa Muda Mrefu.
Marehemu
alishikizwa (Seconded) kwenye wakala wa ndege za serikali hadi alipo
staafu jeshi akiwa na cheo cha Meja December mwaka 2000. Marehemu akiwa Rubani wa ndege alipata nafasi ya kuwarusha viongozi mashuhuri kama:-
i) Marehemu Mwal. Julius K. Nyerere.
ii) Marehemu Nelson Mandela.
iii) Marehemu Pope John Paul II.
iv) Raisi Mstaafu Alhaji Alhasan Mwinyi
v) Raisi Mstaafu Benjamin W. Mkapa Na viongozi wengine wengi wa kitaifa na wakimataifa.
Marehemu
alipata fursa ya kushikizwa katika kampuni ya Williamson Diamond kama
Rubani, pia Kahama Mining na baadae alifanya kazi nje ya nchi Darfur,
Sudan na DR Congo. Marehemu katika siku zake za mwisho alifanya kazi katika shirika la Air Tanzania hadi mauti yalipo mkuta.
Marehemu
alianza kuugua mwanzoni mwa mwezi Januari, 2014 na alitibiwa katika
hospitali mbalimbali hadi mauti yalipo mkuta tarehe January 28 ya mwaka
2014. Marehemu ameacha mke na Watoto wa kiume wane na Watoto wa kike wawili.
SHUKURANI.
Mahospitali – regency hospital, Madakitari na wauguzi hasa Dr. Alfonsi, Dr. Kisanga, na madakitari wa hospitali ya jeshi Lugalo.
Uongozi wa ATC Uongozi
wa Jeshi la wananchi wa Tanzania walioridhia marehem kuzikwa kwa
Heshima za kijeshi, maafisa na maaskari walioshiriki katika paredi za
Mazishi, ndugu jamaa na marafiki walioshiriki kwa hali na mali
kufanikisha katika kumpumzisha baba yetu mpendwa .
0 comments:
Post a Comment