Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza mhifadhi wa Sokwe wa kimataifa
Dkt.Jane Goodall wakati mhifadhi huyo alipomtembelea Rais Ikulu na
kumwelezea kazi zake mbalimbali za uhifadhi nchini. Dkt.Goodall
anajihusisha na uhifadhi wa Sokwe katika hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma
na kazi yake imeipatia Tanzania umaarufu mkubwa Duniani.
Dkt. Goodall ni mwanzilishi wa taasisi ya Jane Goodall Institute inayojihusisha na uhifadhi wa Sokwe.
Picha na Freddy Maro
0 comments:
Post a Comment