Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, amesema Serikali
itapunguza gharama za kukopa fedha kwa riba katika taasisi za fedha na
benki nchini, baada ya Benki ya Rasilimali (TIB) kuingia makubaliano na
Benki ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, katika kutoa mikopo isiyokuwa
na riba kwa miradi yote ya maendeleo ikiwamo ya sekta ya uchukuzi.
Dk Mwakyembe aliyasema hayo jana wakati benki hizo
mbili ziliposaini mkataba wa ushirikiano mwema wa kuwekeza katika sekta
ya uchukuzi.
Alisema kupitia ushirikiano huo, Serikali
itapunguza kukopa katika benki na taasisi za fedha zenye riba kubwa na
badala yake, itatumia fursa hiyo kukopa kutoka TIB kwa ajili ya miradi
yote ya maendeleo ikiwemo miundombinu.
Alisema hiyo itasaidia kupunguza mzigo mkubwa kwa Serikali katika kukopa.
“Kusaini kwa makubaliano haya ni mapinduzi makubwa hapa nchini kwa sababu Serikali itapata unafuu katika bajeti yake,” alisema.
Dk Mwakyembe alisema katika kipindi cha mwaka 2005
hadi sasa Benki ya DBSA, imetoa Dola 130 milioni za Marekani katika
miradi ya miundombinu, huduma za kifedha, huduma za usafirishaji na
mawasiliano hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa TIB, Peter Noni, alisema kwa
kipindi kirefu uongozi wa benki hiyo umekuwa katika majadiliano na DBSA
kwa lengo la kupata fedha za kuendeshea miundombinu katika sekta ya
uchukuzi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa DBSA, Patrick Dlamini
alisema benki hiyo ni taasisi ya kifedha ya Serikali ya Afrika Kusini na
kwamba imelenga katika kusaidia miradi mikubwa.
Chanzo;Mwananhi
Chanzo;Mwananhi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment