Richard Ndassa.
Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Richard Ndassa, aliwaambia waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam jana kuwa, wamebaini wizi huo wakati wa ziara ya kamati yake iliyofanyika katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, hivi karibuni.
Ziara ya kamati hiyo, ambayo ilifanyika katika mikoa ya Mwanza, Simiyu na Shinyanga, ililenga kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali, ikiwamo Rea ya awamu ya kwanza na ya pili, Mpango wa Kukabili Changamoto za Milenia (MCC) na ule wa Electricity Five unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB).
Ndassa, ambaye pia ni Mbunge wa Sumve (CCM), alisema mkandarasi huyo amekuwa akiwatoza wananchi fedha hizo bila kuwapa stakabadhi.
Alisema wizi huo umekuwa ukiwavunja moyo na kuwakatisha tamaa wananchi, hasa wanapojikuta wakitakiwa pia kulipa tena Sh. 32,000 kugharimia huduma ya kuunganishiwa umeme.
Ndassa alisema wizi huo waliushuhudia katika vijiji vitatu, kikiwamo cha Mwankata, kilichopo Jimbo la Msalala, mkoani Simiyu.
Kutokana na wizi huo, alisema kamati imeagiza wananchi wote waliouziwa nguzo, waorodheshwe na kupelekwa kwa Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa ajili ya kurejeshewa fedha zao.
Alisema katika ziara hiyo, pia walipokea malalamiko ya wananchi kupitia Mkuu wa Mkoa huo, Paschal Mabiti, kuhusu ucheleweshaji wa miradi ya umeme unaofanywa na Kampuni ya Symbion, ambayo imekuwa ikijitetea kuwa imepewa miradi mingi na serikali, huku ikiwa haijalipwa.
Ndassa alisema tatizo lingine walilolibaini katika ziara hiyo, ni uhamasishaji mdogo kwa wananchi juu ya kuchangamkia miradi hiyo na uchache wa vifaa, unaochangiwa na vile vilivyoharibika kuchukuwa muda mrefu kufanyiwa matengenezo.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment