Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda.
Rai hiyo ilitolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda, wakti wa ufunguzi wa kituo cha mikutano cha BNN jijini Dae es Salaam na kuwataka kuhakikisha wanalipa kodi kwa maendeleo ya taifa kama mojawapo ya vyanzo muhimu vya mapato ya nchi.
Dk. Kigoda alieleza kuwa kadiri uchumi wa nchi unavyokuwa na maendeleo kuongezeka, mahitaji ya biashara na huduma yanaongezeka, hivyo ni muhimu kuangalia mbinu bora kwa maendeleo ya taifa na kwa ajili ya kuongeza tija na uzalishaji.
“Hakuna nchi yoyote duniani inayojiendesha bila wafanyabishara kulipa kodi, hivyo ni lazima kulipa kodi stahiki kulingana na bishara unayoifanya na pia tuelewe kukwepa kulipa kodi ni kinyume na sheria,” alisema Waziri Kigoda.
Alisema serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa ajili ya kuendeleza biashara na uwekezaji ingawa changamoto bado ni nyingi, lakini zinafanyiwa kazi kwa kushirikiana na taasisi za sekta binafsi.
Pia, Waziri Kigoda aliipongeza sekta binafsi nchini kwa kuwezesha kutoa ajira kwa vijana na kupunguza tatizo la ukusefu a ajira ambalo kwa sasa ni changamoto kubwa katika nchi nyingi duniani.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment