Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Chadema imekosoa uamuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said
Meck Sadick kuzuia waendesha bodaboda, bajaji na maguta wasifike Posta
kwa kile walichodai kuwa hakufuata kanuni.
Akizungumza jana, Dk. Wilbrod Slaa alisema uamuzi
huo aliuita ni batili kwa kuwa alitakiwa kukaa mezani na viongozi
wanaoendesha usafiri huo na siyo kutoa kauli yake kwenye vyombo vya
habari bila ya kuwashirikisha wao.
Dk. Slaa alisema Serikali ilitakiwa kukaa na viongozi nao chini ili waweze kutoa mawazo yao ambayo yangeweza kuleta mwafaka.
“Kilichotokea mkuu wa mkoa huyo alitangaza kuwa
vyombo vya usafiri wa bodaboda, maguta na bajaji zisifike Posta, badala
yake kila dereva aishie kwenye wilaya yake na hakuna barua ya maandishi
walioandikiwa hii ni batili,” alisema Dk. Slaa.
“Hivyo nimeongea na mkuu wa mkoa ameniambia kuwa
kesho atakutana na viongozi wenu ili muweze kufikia mwafaka wenu na nina
imani mtaelewana endapo mtashindikana nawaomba mrudi kwetu ili
tujadiliane,”alisema Dk. Slaa.
Alisema haingii akilini kuona Serikali inachukua
kodi kutoka kwao. Hivyo wanatakiwa wawaachie waendelee kufanya biashara
hiyo hadi hapo mwafaka wao utakapopatikana.
“Hivyo kama Serikali inaamini kuna utawala bora,
naamini watawaachia wale wote waliokamatwa kutokana na makosa ya kufika
posta,” alisema
Chanzo;mwananchi
0 comments:
Post a Comment