Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Jukwaa la Katiba Tanzania imetoa
mapendekezo kwa Serikali kuahirisha uchaguzi wa Serikali za mitaa ili
ufanyike pamoja na uchaguzi mkuu mwakani.
Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Deus Kibamba alisema
uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu ni lazima
uahirishwe kutokana na kucheleweshwa kwa ratiba ya mchakato wa Katiba
Mpya.
Kibamba alisema, Katiba haiwezi kupatikana ndani
ya muda uliokuwa umeahidiwa hapo awali na Rais Jakaya Kikwete Aprili 26,
mwaka huu, kutokana na kubadilika kwa ratiba nzima ya mchakato huo.
Alisema kusogezwa mbele kwa uchaguzi huo kutatoa
muda wa kuandaa sheria za kusimamia chaguzi hizo kwa kuwa Katiba Mpya
pekee haitoshi kusimamia uchaguzi.
Aliongeza kuwa Jukwaa limependekeza nafasi za
wagombea wa Serikali za mitaa kujumlishwa na zile za Uchaguzi Mkuu za
Rais, mbunge na diwani. Zoezi hilo alisema litapunguza gharama za
uchaguzi na muda ambao utatumika.
“Nchi jirani kama Kenya walikuwa nafasi sita za
kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana na Zimbabwe walikuwa
nafasi tano hivyo kwa Tanzania hilo linawezekana kabisa.”
Naye Mkurugenzi wa Sauti za Wanawake Walemavu
Tanzania, Stella Jailos alisema ana wasiwasi kuwa Katiba Mpya haitakuwa
na sura ya wananchi kutokana na wanasiasa kuutawala mchakato mzima wa
kuipata.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment