Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wahandisi nchini wamekumbushwa kuwa
makini kwa kutambua viashiria vya hatari na hasara zinazoweza kutokea
katika miradi mbalimbali ya ujenzi wanayoisimamia.
Hayo yalisemwa na Mwezeshaji katika warsha ya
wahandisi hao, Lwitiko Mwalukasa iliyokutanisha wahandisi kutoka vitengo
mbalimbali nchini, zikiwamo idara za Serikali.
Aliwataka kuwa makini na viashiria hivyo, kwani
baadhi vimesababisha hasara ya majanga, ambayo mengine huleta vifo na
uharibifu wa mali.
Alisema kwa asili kazi ya uhandisi ni kubuni na
kutengeneza kitu ambacho hakikuwapo awali, hivyo hutakiwa pia kufikiria
kwamba hatari au hasara zinazoweza kutokana na vitu hivyo na jinsi ya
kupambana nazo.
“Katika warsha hii tumewakumbusha hatua zote
muhimu wanazopaswa kuzifuata kuanzia kipindi cha mradi unapopangwa
kutekelezwa, kuangalia njia za kudhibiti viashiria vya hatari mapema,
wengi wameonyesha kukubaliana na suala hili, hivyo tunaamini
watawaelimisha na wengine katika maeneo yao ya kazi,”alisema Mwalukasa.
Alisema wahandisi hao iwapo watakuwa makini
watasaidia mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwezesha miradi
wanayoisimamia kukamilika kwa kiwango kinachokubalika na katika thamani
ya fedha iliyotumika, hivyo kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake.
Kwa upande wake, Rais wa Taasisi ya Wahandisi
nchini, Dk Malima Mkandara alisema wameandaa warsha hiyo kuendelea
kuwajengea uwezo wahandisi wa ndani ili waweze pia kushindana hadi
kwenye soko la Kimataifa, hali kadhalika waweze kujipatia kazi za miradi
mbalimbali ambayo inatekelezwa nje ya nchi.
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment