Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Polisi wa Kanda ya Dar es Salaam wamewakamata watu wawili wenye
asili ya Kiasia ambao wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya utekaji
nyara.
Watu hao wanatuhumiwa kutaka kuwateka watoto
wawili wa kike wa mfanyabiashara Aunally Jaffer anayeuza simu Mtaa wa
Samora Dar es Salaam.
Kamanda wa kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova
alisema walipata taarifa hizo Machi 14 mwaka huu na walipochunguza
wakabaini kuna mpango ulioandaliwa na wafanyabiashara waliokuwa na lengo
la kuwateka watoto hao, ili kujipatia Sh5 milioni kutoka kwa wazazi,
ndugu na jamaa zao.
Alisema watoto waliolengwa kutekwa na watuhumiwa
hao ni Shamima Aunally na Halifa Aunally wote ni wakazi wa eneo la
Kisutu na Zanaki.
“Watuhumiwa walioandaa mpango huo ni
mfanyabiashara mkazi wa Kariakoo, Adil Yusuf na mkazi wa Mtaa wa
Jamhuri, Mehul Kava,” alisema Kamanda Kova.
“Walikamatwa wakiwa tayari kuwachukua mabinti hao
ili waondoke nao, lakini polisi walishaweka mtego na kuwakamata eneo la
Jet kabla ya kutimiza azma yao.”
Kamanda Kova alisema walipohojiwa walikiri kuwa lengo lao lilikuwa kujipatia fedha kupitia utekaji nyara huo.
Alisema uchunguzi unaendelea na jalada lipo kwa
Mwanasheria wa Serikali, ili kuthibitisha mashtaka dhidi yao kabla ya
kufikishwa mahakamani.
Alisema kwa sasa wasichana hao na familia yao wapo salama na wanashukuru kwa ushirikiano uliofanikisha kukamatwa kwao.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment