Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wapo hatarini kuathirikia kiafya baada ya kugundulika wanakula nyama ambazo hazijapimwa.
Akizungumza na NIPASHE, Mkuu wa Kitengo cha cha Mifugo Manispaa ya
Kinondoni, Dk, Patricia Henjewele, alisema tatizo hilo linatokana na
upungufu wa wataalamu wa upimaji, usafirishaji duni na ukosefu wa
vitendea kazi.
Dk. Henjewele alisema watu walio katika hatari zaidi ya kula nyama
zisizofaa ni wale wanaokula katika kumbi za starehe, vioski na sehemu
za wazi kutokana na nyama nyingi kutopimwa na wataalam.
Kwa upande wa Kinondoni changamoto ya upungufu wa wataalamu
inasababisha kutofikia malengo ya ufuatiliaji wa kutosha katika maeneo
hayo pamoja na uchakavu wa machinjio ya wanyama.
Alitolea mfano wa machinjio yaliyochakaa kuwa ni Tegeta karibu na
kiwanda cha kuzalisha umeme cha IPL, Kimara Suka, na machinjio ya Eunius
Yusuph yaliyopo Kimara.
Dk. Henjewele, alisema nyama zinazopatikana kwenye kumbi na baa
jijini huo zinachinjwa usiku kwenye maeneo ya makazi ya watu, hivyo
wataalamu wanashindwa kuzikagua kama wanyama hao ni salama kwa matumizi
ya binadamu.
“Wakazi wa jiji hili wanatakiwa kuwa makini na ulaji wa nyama hovyo
hasa kwenye baa,watu waangalie pale ilipotundikwa nyama ya mbuzi au ya
ngombe je imepigwa mhuri, kama hakuna waachane nazo watoe taarifa ili
wachukuliwe hatua za kisheria wahusika.”alisema.
Alisisitiza kwamba kwa kawaida wanapokagua nyama hizo machinjioni
wanapogundua mnyama ana magonjwa ya ini na mapafu,wanatoa amri ya
kufukiwa ili kuzia madhara kwa watu.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment