Home » » MABASI 280 YAPULIZIWA DAWA UBUNGO

MABASI 280 YAPULIZIWA DAWA UBUNGO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Zaidi ya mabasi ya abiria 280 yanayokwenda mikoani na nje ya nchi kutoka kituo kikuu cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam, yameshapuliziwa dawa kuwalinda abiria dhidi ya ugonjwa wa dengue.
Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchikavu (Sumatra), Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Taboa na polisi watakusanyika kituoni hapo kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa zoezi hilo.

Mabasi ambayo yatakuwa yametii agizo hilo hubandikwa stika yenye nembo za jiji hilo, Sumatra na Taboa na kwa yale ambayo hayakutii au yalikuwa bado hayajapuliziwa, hayataruhusiwa kufanya safari zao.

Mweka hazina wa Taboa, Issa Nkya, alisema, hadi jana mchana idadi hiyo ya mabasi yalikuwa yameshapuliziwa dawa hiyo ikiwa ni utekelezaji wa agizo alilolitoa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, kudhibiti ugonjwa huo kwa abiria.

Afisa Afya wa Kituo cha Ubungo, Richard Katiti, alisema kazi ya kupulizia dawa ilikuwa ya siku zote na ipo chini ya sheria ya afya ya umma ya mwaka 2009 kifungu namba 30 (1) ambacho kinatoa amri kwa kila mwenye chombo cha usafiri kufanya hivyo.
 
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa