Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » CHADEMA YAKANA VIONGOZI WAKE KUHAMIA ACT

CHADEMA YAKANA VIONGOZI WAKE KUHAMIA ACT

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
John Mnyika
Chama Cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema) Jimbo la Ubungo kimekanusha uvumi wa taarifa zilizoenea kwamba, aliyekuwa mwenyekiti pamoja na viongozi wengine wa jimbo hilo wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha ACT.
Mwenyekiti wa Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) la Chadema Jimbo hilo, Gaston Shundo, alisema taarifa hizo ni za uzushi na kwamba, zinasambazwa kwa lengo la kuwaonyesha Watanzania kuwa chama hicho kinasambaratika wakati kiko imara.

Alisema kilichotokea kwenye mkutano wa viongozi pamoja na wanachama ni makubaliano ya kuvunja kamati tendaji ya jimbo pamoja na timu ya M4C ili kuunda timu ya msukumo, ambayo ilikabidhiwa majukumu ya kukamilisha uchaguzi wa ndani ya chama jimbo hilo.

“Ikumbukwe kuwa Chadema tunafanya uchaguzi wa ndani ya chama. Na hadi tunafikia makubaliano ya kuundwa kwa timu ya msukumo, Jimbo la Ubungo lilikuwa tayari limekamilisha uchaguzi wa kata nne, ambazo ni Kibamba, Sinza, Makuburi na Manzese,” alisema Shundo.

Alisema timu ya msukumo iliyoundwa, hadi jana ilikuwa imefanya uchaguzi wa kata sita, ambazo ni Ubungo, Saranga, Msigani, Mbezi, Kimara na Goba.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa