Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » UJENZI KITUO KIPYA CHA DALADALA UBUNGO WASUASUA

UJENZI KITUO KIPYA CHA DALADALA UBUNGO WASUASUA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki
 
Ukamilishwaji wa ujenzi kituo kipya cha daladala Ubungo bado kitendawili kutokana na kasi yake kuwa ndogo kinyume cha agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, aliyetaka uwe umekamilika ndani ya wiki mbili, kuanzia Mei 21, mwaka huu.
Sadiki alitoa agizo hilo alipokwenda kukagua kituo hicho wakati madereva wa daladala zinazofanya safari Ubungo-Tegeta kupitia Mwenge kugoma.

Kusuasua kwa ujenzi wa kituo hicho kumeshuhudiwa na NIPASHE jana, ikiwa imepita miezi mitatu tangu agizo hilo litolewe na Sadiki.

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni inayojenga kituo hicho ambao hawakutaka kutaja majina yao walisema hata kwa miujiza hakitaweza kukamilika ndani ya miezi mitatu kwa kuwa ujenzi wake hauwezi kufanywa kwa siasa, bali kitaalamu.

“Kukamilika ujenzi wa kituo mpaka kukabidhi, kunatakiwa kufanya mambo mengi. Ni lazima uhakikishe kituo kina huduma zote za kijamii na mazingira rafiki ya kupokea abiria,” alisema.

Wafanyakazi hao walifafanua kuwa tangu kutolewa agizo hilo wamekuwa wanafanya kazi usiku na mchana, lakini wakasema haiwezekani kukamilika ndani ya siku zilizotolewa na mkuu wa mkoa.

Wakizungumzia adha wanayoipata kwa kuchelewa kukamilika ujenzi wa kituo hicho, baadhi ya madereva wa daladala zinazofanya safari zake Ubungo-Tegeta kupitia Mwenge walisema wamekuwa wakipata tabu, kwani wanatakiwa kugeuzia kituo cha Ubungo Songas na kurudi tena kituo cha darajani.

Chacha Kaloli, ambaye ni Mwenyekiti Msaidizi wa Madereva wa Daladala za Tegeta Ubungo anasema: “Tumekubaliana tutumie kituo cha darajani kwa muda wa wiki mbili. Ila naona hakuna uhakika wa kuanza kutumia kituo kipya kama tulivyoahidiwa,” alisema Chacha.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gunini Kamba, alisema bado wanaendelea kufuatilia ili kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa viwango vyenye ubora.

“Kama umefika, utakuwa umeona ujenzi upo katika hatua ya lami. Kilichofanyika ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za usafiri ” alisema Kamba.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa