Na Andrew Chale
ASIA
Idarous Khamsin na Safari Carnival wanakuletea usiku wa Khanga Party
na Spice Modern Taarab watakaowasha moto wa burudani sambamba na gwiji
wa mipasho nchini Khadija Kopa pamoja na Bilal Mashauzi, Jumamosi ya
usiku wa Novemba 29, ndan ya ukumbi wa Safari Carnival, Mikocheni B.
Kwa
mujibu wa mmoja wa wandaaji wa usiku huo, Asia Idarous Khamsin,
amesema tayari maandalizi yake yamekamilika na amewasihi wadau
kujitokeza kwa wingi katika onesho hilo la aina yake kwa kiingilio cha
sh 10,000 na 20,000 kwa V.I.P.
Asia
Idarous Khamsin alisema Usiku wa Khanga, itaanza kuanzia usiku wa saa
mbili na kuendelea huku vazi maalum likiwa ni Khanga.
"Usiku
huu ni maalum kulienzi vazi la khanga, ambalo pia ndilo vazi maalum la
usiku huo. Pia watafurahia muziki mzuri kutoka kwa magwiji wa taarab
hapa nchini akiwemo Khadija Kopa, Spice Modern taaba na Bilal Mashauzi."
alisema Asia Idarous Khamisin ambapo pia alisisitiza vazi la khanga ni
la heshima hasa kwa mwanamke wa Kitanzania hivyo kila mmoja
atakapolitengeneza vizuri ama kufunga litamweka malidadi.
Aidha,
alibainisha kuwa, usiku huo pia kutakuwa na zulia jekundu 'Red Carpet'
ambapo watu mbalimbali watapata kupiga picha na mastaa na watu maalufu
watakao jitokeza usiku huo.
Pia
alibainisha kuwa, tayari tiketi zimeanza kuuzwa sehemu mbalimbali
jijini Dar es Salaam ikiwemo Fabak fashions Mikocheni na Safari Carnival
kwa mawasiliano piga 0754263363 au 0713263363
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment