Home » » HOSPITALI YA TEMEKE YATUPIWA LAWAMA

HOSPITALI YA TEMEKE YATUPIWA LAWAMA

BAADHI ya wananchi walioshiriki kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Mtoni kwa Aziz Ali, wamewatupia lawama baadhi ya madaktati wa Hospitali ya Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam.

Wananchi hao wamedai baadhi ya madaktari wa hospitali hiyo, huwalazimisha wagonjwa kwenda kununua dawa katika maduka yaliyopo nje ya hospitali hiyo.

Wakizungumza mbele ya Mbunge wa Temeke, Bw. Abbas Mtemvu kwenye Uwanja wa Sifa, walisema changamoto nyingine wanayoipata hospitalini hapo ni watumishi kutowajibika ipasavyo kwa wagonjwa.

“Daktari anakuelekeza uende kununua dawa kwenye maduka yaliyopo nje ya hospitali...suala hili limetuchosha kutokana na sintofahamu iliyopo, maduka hayo ni yao au,” alihoji mwananchi mmoja katika mkutano huo.

Alisema tatizo lingine ni baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo kutokuwepo katika maeneo yao ya kazi; hivyo wagonjwa hulazimika kukaa muda mrefu bila kupata huduma.

Mwenyekiti wa CCM wilayani humo ambaye aliwanadi wagombea wa chama hicho katika uchaguzi huo, Bw. Yahaya Sikunjema, alisema changamoto zilizopo hospitalini hapo zinawakera wagonjwa wanaokwenda kufuata huduma.

Alilitaja Jeshi la Polisi wil ayani humo kua cha kuwaonea waendesha pikipiki zinazobeba abiria ‘bodaboda’ akidai Bunge limeridhia vijana wajiajiri kupitia kazi hiyo sasa iweje wazuiwe kuingia mjini?

“Mbunge tunakuomba uhakikishe vijana wetu wanaendelea kujiajiri kupitia pikipiki wanazoendesha bila kubughudhiwa, wakiendelea kunyanyaswa tutaandamana, hatuogopi kukamatwa na kwenda Segerea.

“Haiwezekani vijana waendelee kupoteza maisha kwa sababu ya kukimbizwa na askari wanaotaka kuwakamata wakiwa kazini ili waweze kujitafutia riziki,” alisema.

Bw. Mtemvu aliyapokea maombi hayo na kuwataka wananchi wajitokeze kwa wingi siku ya kupigakura Desemba 14 mwaka huu ili kuchagua Wenyeviti wa Mitaa ambao atafanya kazi nao.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wilayani humo, Yona Patrik na mkewe juzi walirudisha kadi zao na kuhamia CCM akisema chama hicho hakifai kuongoza nchi kutokana na ubinafsi uliopo.

Chanzo:Majira

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa