Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa
hotuba fupi kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza katika Ufunguzi
wa Mafunzo ya Jinsia kwa Maafisa, Askari na Watumishi raia wa Jeshi la
Magereza, leo Desemba 29, 2014 katika Ukumbi wa Rombo Green View Hotel.
Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku mbili ambapo yatafungwa rasmi kesho
Desemba 30, 2014(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kato Rugainunura(wa pili kulia) ni Mkuu
wa Magereza Mkoani Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza,
Augustino Mboje(kulia) ni Mkuu wa Mafunzo ya Kijeshi wa Magereza,
Kamishna Msaidizi wa Magereza, Mbarak Semwenza.
Baadhi ya Maafisa, Askari na Watumishi raia wa Jeshi la Magereza
wanaoshiriki Mafunzo ya Jinsia katika Ukumbi wa Rombo Green View Hotel
wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi. Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku
mbili ambapo yatafungwa rasmi kesho Desemba 30, 2014.
Mshiriki wa Mafunzo ya Jinsia kutoka Makao Makuu ya Magereza, Mkaguzi
wa Magereza, Amina Lidenge akijitambulisha kabla ya Ufunguzi rasmi wa
Mafunzo ya Jinsia
Mtoa Mada wa Kwanza kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi.
Magreth Mussai akiwasilisha Mada yake kuhusiana na dhana ya Jinsia kama
anavyoonekana katika picha.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma
Malewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa, Askari na
Watumishi raia wa Jeshi la Magereza(waliosimama) mara baada ya Ufunguzi
rasmi wa Mafunzo ya Jinsia leo Desemba 29, 2014 katika Ukumbi wa Rombo
Green View Hotel, (kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kato Rugainunura, (wa pili
kushoto) ni Mtoa Mada wa Kwanza kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na
Watoto, Bi. Magreth Mussai(wa pili kulia) ni Mkuu wa Gereza Kuu la
Wanawake Kingolwila, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Loyce Luhembe,
(kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa Magereza, Augustino Mboje(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la
Magereza).
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment