Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kama hali ya
kuwaengua wagombea wa chama hicho katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa
itaendelea kama ilivyo sasa, basi wataupinga uchaguzi huo mahakamani.
Mbowe alisema hayo jana katika mkutano wa hadhara wa operesheni mshikemshike mzizima uliofanyika Vijibweni Kigamboni.
“Tangu kampeni zianze kumekuwa na tabia ya kuengua
wagombea wetu kiholela. Tumeshaweka angalizo mahakamani na kama hali
ikiendelea hivyo tutaupinga uchaguzi mahakamani.”
Alisema baada ya kuibuka kwa tabia ya wagombea
kuenguliwa aliwasiliana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsihi alitizame
kwa kina suala hilo kwa sababu wagombea walienguliwa kimakosa.
“Alisema atalifanyia kazi lakini naona bado hali
hiyo inaendelea na alisema atazungumza na Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana kuhusu jambo hili.
Nilipowasiliana naye mara ya pili alisema kama
tunataka ushindi uchaguzi uwe wa haki. Kuona hivyo tumekwenda kutoa
angalizo mahakamani,” alisema.
Aliongeza, “Tukutane katika uchaguzi na tuone nani
ni bingwa kati ya CCM na Ukawa baada ya kutumia njia za mkato kama wao
wanavyofanya.
Hata sisi hatutaki ushindi wa dezo ila wakitumia
dola kutuyumbisha kamwe hatutokubali maana polisi wamekuwa wakitumika
kama mawakala wa uchaguzi. Hilo halitakubalika.”
Aliwataka wananchi kutokaa mbali na vituo vya
kupigia kura mara baada ya kuwachagua viongozi wanaowataka huku
akisisitiza, “Msikubali kura zikahesabiwe sehemu nyingine
watazichakachua.
Hata katika sheria za Uchaguzi hakuna sehemu
inayosema baada ya kupiga kura, mpigakura anatakiwa kukaa umbali wa mita
100 kutoka katika kituo cha kupiga kura. Tumeweka mawakala nchi nzima
kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa.”
Alisema hakuna dhambi mbaya kama wananchi
kushindwa kuleta mapinduzi ndani ya nchi yao, hasa nchi kama Tanzania
ambayo ina kila aina ya umasikini.
Chanzo;Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment