Maalim Hassan Hussein, ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mtabiri
maarufu nchini, marehemu Sheikh Yahya Hussein, ametabiri mambo 18
yatakayotokea mwakani, likiwamo la kufariki ghafla kwa kiongozi mmoja
mzee ambaye yumo kwenye mbio za urais mwakani.
Hussein alisema jana kuwa kiongozi huyo atadondoka
ghafla kwenye jukwaa na kufariki dunia wakati akipelekwa
hospitali.Akitangaza utabiri wa mwakani, alisema: “Kiongozi huyo atakufa
wakati akipelekwa hospitalini.”
Alisema pia mwandishi mmoja mashuhuri nchini
atakufa kifo chenye utata kitakachoitesa Serikali na familia yake katika
kutafuta sababu za kifo chake.
Mtabiri huyo alisema nyota inaonyesha kwamba misiba miwili ya kitaifa itatokea mwakani.
Kuhusu uchaguzi wa kiti cha urais mwaka 2015,
alisema kati ya kundi la vijana na wazee, nyota zinaonyesha kwamba
watakaofaidika ni vijana.
“Lakini kuna wazee pia wanaoweza kufaidika, hawa
ni wale wenye sura za ujana, yaani babyface au wenye kupenda mambo ya
ujana na kushirikiana na vijana,” alisema.
Alisema ili Tanzania ilinde sifa ya kuwa nchi
yenye amani na utulivu ni kuwa na Rais kijana mwenye mchanganyiko wa
dini mbili au mwenye ndoa ya dini tofauti.
Alisema utabiri unaonyesha kuwa mwaka 2015
utatawaliwa na nyota yenye kupendelea vijana, hivyo ni vyema vyama vya
siasa vikawasimamisha kugombea nafasi za urais, ubunge na udiwani.
Kuhusu mauaji, fujo na ghasia alisema vitatawala katika uchaguzi ujao na kwamba Serikali inatakiwa kuweka tahadhari kubwa.
Pia alitabiri viongozi wawili wa siasa na dini
kukumbwa na kashfa ya ngono itakayowasababisha anguko la utumishi wa
kutukuka na familia zao.
Alisema mwaka ujao utakuwa na mafuriko na dhoruba vitakavyosababisha madhara, hivyo tahadhari ichukuliwe kuanzia sasa.
Alisema kutakuwa na vifo vya ghafla vya wasanii, wanamichezo na watu maarufu kama ilivyokuwa mwaka 2014.
Maalim Hussein alisema lile tishio la wahisani kuiwekea Tanzania
vikwazo vya kiuchumi, litalegezwa na kuifanya nchi kuingia katika
Uchaguzi Mkuu kwa staha.
Alisema wazee wataendelea kushutumiana na
kupingana hadharani, hali itakayosababisha migawanyiko ndani ya vyama
vya siasa na nchi kwa jumla.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment