Home » » LAAC YAMWEKA KITIMOTO MWANASHERIA WA KINONDONI

LAAC YAMWEKA KITIMOTO MWANASHERIA WA KINONDONI

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imetoa onyo kali kwa Mwanasheria wa Halmashauri ya Manispaa Kinondoni, Grace Makowa, kwa kuwadhalilisha wabunge kwa kile kilichoelezwa kuwaita wabunge waongo.

Wabunge hao walitoa onyo hilo wakati Kamati hiyo ilipokutana na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa Kinondoni Dar es Salaam jana kwa ajili ya kutolea ufafanuzi hoja mbalimbali zilizokuwa zikiulizwa na wabunge hao.

Mwenyekiti wa Kamati ya LAAC, Rajab Mbarouk alisema kitendo cha mwanasheria huyo kudharau wabunge ni sawa na kumdharau Rais Jakaya Kikwete, ambaye amewatuma kazi hiyo.

"Tunamtaka ajipime kama anastahili kuendelea kufanya kazi hiyo," alisema Mbarouk. Pia wabunge wa kamati hiyo walionekana kukerwa na utendaji wa ofisi ya mwanasheria wa Kinondoni na kusema kwamba imejaa uozo, hivyo haimsaidii mkurugenzi katika utendaji kazi wake.

Alisema kamati hiyo imebaini kutafunwa fedha za miradi 11 kati ya 15 iliyokuwa ikitekelezwa katika wilaya hiyo, lakini hakuna majibu yanayojitosheleza kuhusiana na sababu ya hali hiyo.

Alisema miradi hiyo 11 kwa jinsi ilivyotekelezwa haina uwiano na miradi husika.

Chanzo:Majira

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa