Home » » MGOGORO ATC-TANZANIA: UAMUZI NI BATILI- MWANASHERIA

MGOGORO ATC-TANZANIA: UAMUZI NI BATILI- MWANASHERIA

SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Mabadiliko na Uwazi (ACT-Tanzania), Kadawi Limbu, kutangaza kuwavua uanachama baadhi ya viongozi wa chama hicho, uamuzi huo unadaiwa kuwa batili.

Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Mwanasheria wa chama hicho, Thomas Matatizo, alisema viongozi wote waliofukuzwa katika chama na kuvuliwa uanachama wataendelea na nyadhifa zao.

Alisema maamuzi yaliyotangazwa na Limbu ni batili kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho na Sheria ya Vyama vya Siasa.

Aliongeza kuwa, hakuna Kikao cha Kamati Kuu kilichokutana katika tarehe iliyotajwa na Limbu bali kikao hicho kimepangwa kufanyika Januari 5, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

“Maamuzi yaliyotangazwa juzi na Limbu kuwavua uanachama Katibu Mkuu, Samson Mwigamba na Mshauri wa chama Profesa Kitila Mkumbo ni batili...viongozi hawa na wengine waliovuliwa uanachama wataendelea na nyadhifa zao.

Matatizo alisema mkutano alioufanya Limbu, alidai maamuzi ya kuwavua uanachama viongozi hao yalifikiwa kwenye Kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Desemba 30,2014, jambo ambalo si la kweli.

“Jukumu la kuandaa ajenda za vikao vya Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba ya chama ibara ya 37 q(iii) lipo kwa Sekretarieti ya chama si vinginevyo,” alisema.

Juzi Limbu akiwa na viongozi wengine wa chama hicho, aliitisha kikao na waandishi wa habari na kutangaza kuwavua uanachama Mwigamba, Prof. Mkumbo, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara, Shaban Mambo, Mwenyekiti wa Wazee Wilson Muchumbusi na Katibu wa Vijana, Philip Malaki.

Katika maelezo yake, Limbu alisema Mwigamba na Prof. Mkumbo wamevuliwa uanachama na kufukuzwa kutokana na matumizi mabaya ya madaraka na kukikabidhi chama kwa mafisadi.

Alisema viongozi hao walishiriki kusaini makubaliano ya kuendesha shughuli mbalimbali za chama, kusimamia mikutano ya uchaguzi na kampeni ya Developpement Politique Culture kutoka nchini Senegar bila kushirikisha viongozi wengine.

Chanzo:Majira

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa