Mtibwa Sugar imereja kileleni mwa Ligi Kuu
pamoja na kulazimishwa sare 1-1 na JKT Ruvu jana kwenye Uwanja wa Azam
Complex, Chamazi.
JKT Ruvu ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia
Samuel Kamutu dakika ya sita akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa
Mtibwa, Said Mohamed, kabla ya Ame Ally kuisawazisha Mtibwa Sugar kwa
kichwa akiunganisha kona ya Shija Kichuya.
Matokeo hayo yameifanya Mtibwa Sugar ambayo
haijafungwa msimu huu kufikisha pointi 17 sawa na JKT Ruvu na Azam FC,
lakini ikiongoza ligi kwa tofauti ya mabao.
Mchezo mwingine uliochezwa Tanga, Coastal Union
ilishindwa kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa
suluhu na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Ratiba ya Ligi Kuu imeingizwa mechi za viporo
zilizotokana na Yanga, Azam, Mtibwa Sugar na Simba kucheza michuano ya
Kombe la Mapinduzi.
Mechi za viporo itakuwa kama ifuatavyo; Januari
20- Kagera Sugar na Azam (Mwanza), Januari 28- Simba na Mbeya City (Dar
es Salaam), Februari 4- Coastal Union na Yanga (Tanga), Februari 11-
Azam na Mtibwa Sugar (Dar es Salaam) na Mgambo Shooting na Simba
(Tanga). Yanga na Ndanda (Dar).
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment