Home » » NEC: KURA YA MAONI ITAFANYIKA APRILI 30.

NEC: KURA YA MAONI ITAFANYIKA APRILI 30.

Zikiwa zimebaki siku 73 kupia kura ya maoni Katiba inayopendekezwa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), ambayo inajukulu la kufanikisha zoezi hilo, imesema imamatumaini kuwa litakamilika.
 
 Hata hivyo, pamoja na Nec kusema hivyo, bado inaonekana inakabiliwa na changamoto nyingi kulifanikisha.
 
Kwa mujibu wa sheria namba tatu ya mwaka 2014 ya kura ya maoni,  jambo la kwanza kufanyika ni uboreshaji wa daftari la wapigakura, elimu kwa umma kwa miezi miwili na kampeni kwa mwezi mmoja.
 
Tayari serikali imetangaza kuwa kura ya maoni kwa Katiba inayopendekezwa itafanyika Aprili 30, mwaka huu.
 
Moja ya mitihani hiyo ni kukamilisha zoezi la uandikishaji wa wapiga kura unaotarajiwa kuanza Februari 16, mwaka huu, kwa kuanza na mikoa mitatu ya Njombe, Ruvuma na Lindi, ambalo litafanyika kwa siku saba kwa kila mkoa.
 
Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva, akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu, alisema Wataanza na mkoa wa Njombe kwa kutumia vifaa 250 vilivyopo wakati wanasubiri vifaa vingine ili waweze kwenda katika mikoa mingine.
 
Alisema zoezi la uandikishaji litaanza Februari 16, hadi Machi 15, mwaka huu, na kwamba ni matumaini ya Tume kuwa zoezi litakamilika kwa mikoa yote kabla ya Aprili 29, mwaka huu.
 
Suala hilo linachukuliwa kama mtihani wa kwanza na mkubwa kwa Tume hiyo kwa kuwa kila mkoa utatumia siku saba ambazo ni sawa na siku 182 kwa mikoa 26 ya Tanzania, kwa Watanzania kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
 
Iwapo zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura litaanza Februari 16, mwaka huu, kwa kila mkoa siku saba kwa kwenda mkoa kwa mkoa litamalizika Agosti 16, mwaka huu.
 
Mtiririko huo unakwenda kinyume cha matarajio na kauli ya serikali kuwa kura hiyo itafanyika Aprili 30, mwaka huu, huku ukiwa ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na rais huku elimu na kampeni kwa Katiba inayopendekezwa haijafanyika.
 
Kwa mujibu wa sheria hiyo baada ya uboreshaji wa daftari hilo, litafuatiwa na elimu kwa umma kwa miezi miwili kisha kampeni kwa mwezi mmoja.
SOURCE: NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa