Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

PSPF WAANZISHA KAMPENI MPYA YA MTAA KWA MTAA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Balozi wa mfuko wa pensheni wa PSPF Mrisho Mpoto Maalufu kama (Mjomba) akitoa burudani pamoja na kutoa elimu kwa wananchi waliofika kupata elimu juu ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa Hiari kupitia kampeni ya mtaa kwa mtaa iliyofanyika jijini Dar
Afisa wa mfuko wa pensheni wa PSPF Hadji Hamis Jamadary akitolea ufafanuzi kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko wa PSPF hasa katika uchangiaji wa Hiari ambapo aliwasisitiza wananchi kuwa kila mwananchi anaweza kujiunga na mfuko huo na kusisitiza hakuna makato yoyote anayokatwa mteja anapojiunga na mfuko huo.

Jeshi la Polisi lawashikilia watuhumiwa kumi na mbili wa wizi wa Makontena.‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na Nyakongo Manyama-Maelezo
Tarehe : 30/11/2015.
Dar es Salaam.

Kufuatia agizo laWaziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kuwataka watuhumiwa wa wizi wa makontena 329 katika bandari ya Dar es salaam kuchukuliwa hatua na Jeshi la Polisi, tayari Jeshi hilo limewashikilia watuhumiwa kumi na mbili wanaohusika na wizi huo.

Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam,  Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CP) Diwani Athumani amesema kuwa, uchunguzi unaofanywa na wataalamu waliobobea katika makosa ya uhalifu wa kifedha umeweza kuwabaini watu kumi na mbili  ambao wamehusika na wizi huo.

“Kati ya watuhumiwa hao kumi na mbili, watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na saba bado wapo katika upepelezi na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani,” alisema Kamanda Athumani.

Wanaoshikiliwa kutokana na tuhuma mbalimbali ni Kamishna wa Idara ya Forodha na Ushuru TRA Bw. Tiagi Masamaki, Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru  na Bi.  Habib Mponezia, Msimamizi Mkuu wa Kitengo cha Ushuru wa Forodha.

Watuhumiwa wengine ni pamoja na Bi. Eliaichi Mrema, Msimamizi Kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta  Bw. Haroun  Mpande na Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara Bw. Hamis Omary.

Aidha Kamanda Athumani amewaomba wananchi wenye taarifa za ubadhilifu wa mali za Umma kuendelea kulisaidia Jeshi la Polisi katika kutekeleza majukumu yake.

    

RAIS DKT. MAGUFULI, WAZIRI MKUU MAJALIWA, WAMTEMBELEA MAKAMU WA RAIS, MHE. SAMIA OFISINI KWAKE IKULU JIJINI DAR

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, (kushoto) akizungumza na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, wakati Rais na Waziri Mkuu walipomtembelea Makamu Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015 kwa mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akiagana na  Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015. Wa pili (kulia) ni Naibu Katibu wa Makamu wa Rais, Mohamed Khamis
Picha na OMR.

Watumishi wa Umma watakiwa kushiriki zoezi la usafi disemba 9‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Shamimu Nyaki-Maelezo

Serikali imewaagiza watumishi wa umma kushiriki zoezi la usafi wa  nchi  litakalofanyika tarehe 9 disemba mwaka huu katika maeneo yao wanaoishi.

Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw Assah Mwambene alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijin Dar es salaam na kusema kwamba Watumishi wa Umma  wanatakiwa wabaki nyumbani na kufanya usafi katika maeneo yao na  yale watakayo pangiwa na viongozi wa mitaa wanayoishi.

“Kila mwananchi ahakikishe eneo lake ni safi”Alisema Mwambene.

Mkurugenzi ameongeza kuwa Watumishi wa Umma hawataenda kazini badala yake  watabaki  nyumbani na kufanya usafi kwa kushirikiana na wananchi kusafisha maeneo yanayozunguka mitaa wanayoishi ikiwemo hospitali,kuzibua mitaro iliyoziba pamoja na kuzoa taka zilizolundikana sehemu ambazo sio rasmi.

Ameongeza kuwa muongozo kuhusu namna zoezi la usafi litakavyotekelezwa umeshatolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI  kwa Uongozi wa Mikoa hadi Mitaa na kilichobaki ni utekelezaji tuu wa agizo hilo kwa kila mwananchi sehemu anayoishi,anayofanyia shughuli nyingine za kila siku kuhakikisha anafanya usafi.

Aidha Mkurugenzi amewataka viongozi wa kila eneo kutengeneza utaratibu mzuri ambao utafanikisha zoezi la usafi  kufanikiwa kwa kuhakikisha wanasimamia kwa ukamilifu na kuwahimiza wananchi kuwa na tabia ya kusafisha maeneo wanaoishi kwa kuwa ni wajibu wao kufanya hivyo.

Hata hivyo tarehe tisa disemba kila mwaka huwa ni siku ya kusherehekea Uhuru wa Tanganyika uliopatikana miaka hamsini na nne iliyopita lakini kwa mwaka huu itaadhimishwa kwa kufanya usafi nchi nzima.

Wizara ya Nishati na madini yaendelea kutekeleza kwa vitendo ahadi za Rais Dkt. Magufuli

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Dola za Marekani Milioni 3.4 Zatengwa Kusaidia Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na. Lilian Lundo – Maelezo

Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imetenga jumla ya Dola za Marekani Milioni 3.4 kusaidia vikundi vya wachimbaji wadogo na watoa huduma  katika migodi nchini.

Akiongea na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini Badra Masoud amesema, hatua hii imekuja baada ya  Serikali kubaini kwamba wachimbaji wengi wadogo huchimba madini kwa kutumia zana na vifaa duni kutokana na ukosefu wa  fedha za kununulia vifaa vya kisasa.

“Wachimbaji wadogo wengi hawawezi kukidhi masharti ya kupata mikopo katika benki za biashara nchini, hivyo Serikali inawajengea uwezo hatua kwa hatua hadi wafikie hatua ya kuweza kukopesheka katika mabenki ya kibiashara,” alisema Badra.

Aidha, Badra alisema kuwa pesa hizo zitatumika kwa miaka mitatu kuanzia mwaka huu wa fedha 2015/16 kwa ajili ya kuwawezesha wachimbaji madini wadogo kupata ruzuku kwa awamu ya tatu ili waweze kuchimba kisasa na kujiongezea vipato vyao na kuongeza pato la Taifa.

Badra alizidi kufafanua  kwa kusema kuwa, ruzuku hii ni jitihada za Serikali katika kukwamua wachimbaji wadogo kuondokana na umasikini kwa kuwajengea uwezo  wa kufikia  kuwa wachimbaji wa kati.

Vilevile Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, imetenga maeneo yenye ukubwa wa hekari 197,432 kwa ajili wa wachimbaji wadogo ili kuendeleza uchimbaji wa madini mdogo nchini.

Serikali itaendelea kuwa karibu na wachimbaji wadogo waliopatiwa ruzuku kuhakikisha fedha wanazopewa wanazitumia kama ilivyokusudiwa na si vinginevyo, wachimbaji hao watapewa elimu ya uchimbaji wa kisasa, utunzaji wa mazingira na namna ya kuepuka ajali ndani ya migodi

MAPACHA WANNE WALITEKA JIJI LA DAR ES SALAAM‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Kiongozi wa Bend ya Twanga Pepeta Rwiza Mbutu akiwa jukwaani wakati wa shoo ya uzinduzi baada ya kujiunga tena katika Bendi ya  mapacha Wanne




 Chazi Baba kulia akiwa na Josee Mara wakiwa katika shoo iliyo wavutia wadau wakati wa uzinduzi wa nyimbo yao ya usiku wa kuachwa iliyozinduliwa hivi karibuni baada ya kusambaratika.
 Mpenzi wa Bend ya Mapacha wanne Fredicto Mupao 'mwana tarime' akimwagia mapesa mwimbaji wa Bend ya Mapacha wanne Kalala Jonia (kulia) katika ukumbi wa Mango Gaden wakati wa usiku wa nyimbo ya kuachwa iliyo zinduliwa hivi karibuni Jijini Dar es Salaam 
 Rwiza Mutu akiwa Jukwaani
 Mdau achanganyikiwa kwa kumwagia mapesa Mwimbaji wa Bend wa ya Mapacha wanne, KalalaJunia baada ya kuvutiwa na kipaji cha uimbaji wa mwimbaji huyo nakujikuta anamwagia mapesa
 Kuanzia kulia ni Chazz Baba, Haridi Chokora, Kalala Junia, Josee Mara
Kuanzi kulia ni Haridi Chokora, Kalala Jnia, Chazz Baba, Josee Mara

Taarifa ya upotevu wa makontena AZAM ICD toka SSB Group of Companies

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Kumekuwa na taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa kampuni ya Bakhresa inahusika na upotevu wa Makontena 349 yaliyoripotiwa hivi karibuni kuwa yametolewa bandarini bila kulipiwa ushuru. Taarifa hizo zilitolewa na Waziri Mkuu wakati wa ziara yake ya Bandari ya Dar es salaam hivi karibuni.
Uchunguzi wetu umeonyesha kuwa si kweli kuwa kuna makontena yenye bidhaa zilizoingizwa na kampuni hio ama ni miongoni mwa makontena yaliyohusika katika sakata hilo. Isipokuwa kumetokea upotevu wa makontena yaliyoingizwa nchini na baadhi ya wafanyabiashara katika eneo la kuhifadhia makontena(ICD) linalomilikiwa na kampuni hiyo la Azam ICD.
Aidha imebainika kuwa kuna uchunguzi unaofanywa na mamlaka ya mapato nchini TRA, huku kukiwa na ushirikiano na uongozi wa Kampuni hiyo (SSB Group of Companies) kuhakikisha wale wote wanaohusika na upotevu huo wanachukuliwa hatua na kodi yote ya serikali inalipwa na wamiliki wote wa makontena yaliyohusika katika upotevu huo wanawajibishwa.
SSB Group of Companies
Corporate Affairs Department
November 29, 2015

KAMPUNI YA MSAMA PROMOTIONS YAMWAGA MISAADA VITUO 10 VYA YATIMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Halima Ramadhani ambaye ni Mkurugenzi wa Kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni Dar es Salaam akipokea msaada wa vyakula pamoja na mahitaji mengine kutoka kwa Alex Msama.
Sehemu ya msaada uliotolewa kwa vikundi 10 vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwa amembeba mtoto, Haidin Edwin wakati wa hafla ya kukabidhi misaada mbalimbali ikiwemo vyakula kwa vikundi 10 vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu, iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwabidhi watoto Haidan Edwin na Gatson Edwin sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali alivyotoa kwa kikundi cha Tuwakomboe cha Temeke jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mapato ya matamasha yaliyopita.


Watoto wakipata vinywaji baridi wakati wakisubiri kukabidhiwa msaada wa vitu mbalimbali kutoka Kampuni ya Msama Promotions.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari.


KAMPUNI ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam chini ya Mkurugenzi wake, Alex Msama, ilikabidhi misaada ya vitu mbalimbali kwa vituo 10 vya kulea watoto yatima ikiwa ni sehemu ya mapato ya matamasha yaliyopita.

Akikabidhi misaada hiyo kwa watoto hao, Msama alisema wamefanya hivyo kwa kutambua nafasi yao katika jamii kwamba, watoto hao wanayo haki ya kupata mahitaji muhimu katika makuzi kama wengine wenye wazazi wao.

Msama alisema msaada huo wenye thamani ya sh. milioni 7.5, ni sehemu ya fedha ambazo zimekuwa zikipatikana kupitia matamasha ya muziki wa Injili ambayo ni wakati wa Pasaka na Krismasi.

“Msaada huu ni sehemu ya fedha ambazo tumekuwa tukizipata kwa njia ya matamasha ambayo tumekuwa tukifanya jijini Dar es Salaam na mikoani; Pasaka na Krismasi,” alisema.

Msama, alisema wamekuwa wakisaidia watoto yatima na makundi mengine maalumu katika jamii kwa kutambua kuwa huo ni wajibu wa kila mmoja na ametoa wito kwa wengine kuwa na moyo wa kusaidia makundi hayo.

Vituo vilivyopata misaada hiyo ni Umra, Zaidia, Hiari, Malaika, Maunga, Mwandaliwa, Sifa, Honoratha, Chakuwama na Rahman vya jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa vitu vilivyokabidhiwa ni unga wa sembe, mchele, unga wa ngano, sukari, sabuni, mafuta ya kupikia, mafuta ya kupaka, dawa za meno na vinginevyo.Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kupokea misaada hiyo ya kiutu, viongozi wa vituo hivyo walisema ni faraja kubwa kwao na watoto hao wenye mahitaji maalumu.

Maombio Jonas, mwakilishi wa Kituo cha Sifa Group Foundation cha Bunju, ametoa shukrani kwa Msama kwa moyo wa kujitolea kusaidia watoto wenye mahitaji na kutoa wito kwa wengine kuiga mfano wa moyo huo wa upendo.

Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Hiari cha Chang’ombe, Aminajat Klemia, alitoa pongezi kwa Msama kutokana na misaada hiyo akisema ni faraja kubwa kwa watoto hao ambao wanahitaji kuthaminiwa kama wengine.

Misaada hiyo imetolewa wakati ambapo kampuni hiyo ipo katika maandalizi ya Tamasha la Krimasi litakalofanyika Desemba 25 kwa ajili ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo pia kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuijalia nchi kuvuka salama katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.

UN WAKISHIRIKIANA NA UBALOZI WA PALESTINA WAFANYA MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA MSHIKAMANO NA WATU WA PALESTINA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima (katikati), Kaimu Balozi wa Palestine Derar Ghannam (kulia) pamoja na Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohammed Ali wakikata utepe kwa ajili ya maonesho ya picha za matukio mbalimbali yanayoendelea nchini Palestina hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar.
Kaimu Balozi wa Palestina Derar Ghannam (wa kwanza kulia) akimuonyesha picha Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima (katikati) za matukio ya mauaji ya watu nchini Palestina yanayofanywa na Waisraeli ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar.
Baadhi ya picha zinazoonesha matukio ya mauaji pamoja na majeruhi yanayoendelea kutokea nchini Palestina kutokana na vita inayoendelea nchini mashariki ya Kati kati ya Palestina na Israeli.
Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi Stella Vuzo (kulia) akitazama picha za wananchi wa Palestina waliouliwa na kutokana na mapigano ya Palestina na Israel yanayosababisha vifo vya watu wengi wasiokuwa na hatia.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiendelea kusikiliza kwa makini wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina. Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima akisoma hotuba yake mbele ya Mabalozi, wanafunzi wa chuo cha Diplomasia pamoja na wageni waalikwa waliofika kwenye maadhimisho ya ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar.
Naibu Mkurugenzi wa Mipango Utawala na Fedha wa Chuo cha Diplomasia, Dk.Bernard Achiula akizungumza jambo wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika chuoni hapo.
Prof Josephat Kanywanyi ,Chairperson Tanzania- Palestine Solidarity committee akitolea ufafanuzi kuhusu mahusiano ya Tanzania na Palestina wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina.
Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohammed Ali akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na watu wa Palestina.
Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia wakiendelea kusikiliza kwa makini kinachozungumzwa kutoka meza kuu.
Mshauri Mwandamizi wa Utawala kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa mataifa (UNDP), Steve Lee aliyemwakilisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza uhusiano wa Palestina na Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar.
Baadhi ya Mabalozi waliofika kwenye maadhimisho hayo wakiendelea kufuatilia yanayojiri.
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya Pamoja na Viongozi mbalimbali pamoja mabalozi.
Viongozi wakiwa kwenye picha na wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia. 

Na Mwandishi wetu
  UN Tanzania ikishirikiana na Ubalozi wa Palestina nchini waadhimisha Siku ya Kimataifa na Mshikamano na watu wa Palestina na Tanzania katika Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma na kukutana na mabalozi wa wa nchi mbalimbali akiwepo Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima, Kaimu Balozi wa Palestina Derar Ghannam na Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohammed Ali ambapo ikiwa kuendeleza ushirikiano pamoja na mfululizo wa maonesho ya picha mbalimbali za matukio yanayoendelea huko nchini Palestina. 
  Mabalozi hao ambao walikutana katika jijini Dar es salaam kwaajili ya kuadhimisha siku hiyo ya kumbukumbu za picha za mapigano ya Palestina kwa ajiri ya kudumisha upendo na mshikamano pia mabalozi hao wameuomba umoja wa mataifa kuweza kuchukua hatua za ziada zitakazo pelekea nchi hiyo kuwa huru na kuweza kuendelea kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo. 
  Mshauri Mwandamizi wa Utawala kutoka UNDP, Steve Lee akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alisema kuwa uhusiano wa Palestina na Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina alisisitiza kuwa na na umoja baina ya nchi zote mbili hususani Palestina kuweza kupata uhuru na kutambulika kuwa ni nchi nyenye mipaka yake binafsi ili kuepusha mapigano hayo yasiweze kutokea na kila mtu aweze kuishi na amani akiwa ndani ya nchi yake na kuweza kufanya maendeleo ya nchi. Na aliweza kuziomba nchi mbalimbali kulitambua taifa la Palestina kama nchi kamili tofauti na inavyotambulika kwa sasa. 
  Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa siku ya maonesho ya picha Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima amesema wamefanya hivyo kwani ni hari ya kuwatakia heri Wapalestine wote kwani watu wote waparestine walipoteza uhuru na kwa sasa wanautafuta uhuru kwani nchi wanayo lakin hawako huru kwahiyo ni lazima tuwaunge mkono kwa kuweza kuadhimisha siku hii sehemu mbalimbali tunayoishi. 
  Kwa upande wa Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UNIC), Bi Stella Vuzo amesema wameamua kuwa na maadhimisho kwani ndani ya miaka 50 Palestina wamekuwa hawajatambulika kama taifa lenye mipaka yake ambapo kumekuwa na migogoro ya mda mrefu ambao unawahusu wa Palestine na wayahudi ambao upo tangu mwaka 1947,wakati katika maadhimio walio fikiana ni kuwa na mataifa mawili ndani ya eneo moja ambap mpaka sasa Israel pekee ndo iliyo pata kuwa hali ya taifa lenye mipaka yake wakati . Kila siku Israel huwa wanaleta vita ndani ya Palestine, sasa maadhimisho haya ni kwa ajili ya kuwaunga mkono kwa vitendo vinavyo endelea huko si vizuri. Pia aliwaomba viongozi wa pande zote mbili kuweza kuketi na kuweza kuweka maadhimio mapya kwaajili ya kuepusha mapigano yanayokuwa yakitokea kila siku baina ya nchi hizo mbili. Pia katika siku hiyo waliweza kuzindua picha za matukio ya vifo pamoja na watu walioumia kutokana na vita Palestina na Israel zilizo kuwa zimeandaliwa kwa Tanzania kwa ajili ya kuonyesha dunia matukio yanayoendelea katika nchi za Mashariki ya mbali hii yote ni kwa kuwa Palestina ina ushirikiano na Tanzania na kuwaombea katika kuelekea hali ya utulivu.

MBUNGE WA JIMBO LA ILALA MSSA ZUNGU ATEKELEZA AHADI ALIYOITOWA WAKATI WA KAMPENI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
  Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu (CCM) (mwenye kofia) akimkabidhi nahodha wa timu ya Ferry Beach Boys, Selemani Ally 'Kaseja' nyaraka za  Pikipiki hiyo Dar es Salaam leo ambayo ilikuwa ni moja ya ahadi yake kwa kikosi hicho wakati wa kampeni.(PICHA NA  KHAMISI MUSSA)
 Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu (CCM) (mwenye kofia) akimkabidhi nahodha wa timu ya Ferry Beach Boys, Selemani Ally 'Kaseja' namba ya Pikipiki Dar es Salaam leo.  

 Zungu amesema  ilikuwa ni moja ya ahadi yake kwa kikosi hicho wakati wa kampeni alipofika kituoni hapo wakati alipopita kumuombea kura aliyekuwa mgombea  Urais Mgufuli  kupitia Chama cha Mapinduzi  CCM  ili iwasaidie kujikusanyia kipato kwa njia hiyo ya kujikusanyia kipato ili wapate nauli wanapokuwa wakienda kucheza kwenye pindi wapatapo mwaliko,   Mbunge huyo aliendelea kusema nitaendelea kusaidia maswala ya timu na alipewa ombi la timu kusaidia vifaa vya michezo  lakini leo nakusaidieni Pikipiki iwe mali ya timu si mali ya mtu, anaendelea kusema Zungu, alitowa ahadi ya Bodi ya Ferry na bodi hiyo ipo tayari  tunasubiri waraka uchapishwe na fikiri kabla ya mwezi wa kumi na mbili kwisha bodi itakuwa imeundwa ili Soko hili liendeshwe na wafanya Biashara wenyewe, na niliweka ahadi ya kuwawekea mahema kwenye maeneo ya wanaouza Samaki maeneo ya wanaopigwa na Juwa na kabla ya mwezi wa kumi na mbili itakuwa tayari.

WAFANYAKAZI WA OFISI YA MAKAMU WA RAIS WAFANYA BONANZA LA KUMUAGA MAKAMU WA RAIS MSTAAFU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya VPO Sports Club, Nehemia Mandia, baada ya kuibuka na ushindi katika Bonanza maalum la kumuaga Dkt. Bilal, lililofanyika jana Nov 28, 2015 kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. VPO waliibuka kidedea baada ya kuwafunga timu ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa mikwaju ya penati 5-4.
  Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha kushiriki Nahodha wa timu ya Kamati ya Amani Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum, katika Bonanza maalum la kumuaga Dkt. Bilal, lililofanyika jana Nov 28, 2015 kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. VPO waliibuka kidedea baada ya kuwafunga timu ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa mikwaju ya penati 5-4.

  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula, akizungumza wakati wa Bonanza maalum la kumuaga Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, liliandaliwa na timu ya timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais (V.P.O Sports Club) lililofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete, uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam jana Nov 28, 205. Katika Bonanza hilo lililoshirikisha jumla ya timu Nne za VPO Sports Club, Wizara ya Mambo ya Nje, Kamati ya Amani waliochanganyika na Mabalozi na Amana Bank waliochanganyika na Zanzibar Fc, Timu ya VPO Sports Club iliibuka na ushindi kwa kuwafunga Mambo ya nje kwa jumla ya mikwaju ya penati 5-4 na kutwaa kombe la Bonanza hilo
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamuuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wanamichezo baada ya kumalizika Bonanza la kumuaga, lililofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete,uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam  jana
 Nahodha wa timu ya VPO Sports Club, Muhidin Sufiani, akimtoka beki wa timu ya Kamati ya Amani, Mhungaji Amos Nene, wakati wa Bonanza maalum la kumuaga Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, lililofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete,uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam  jana Nov 28, 2015. Katika Mchezo huo VPO walishinda kwa bao 1-0 na kutinga fainali na Timu ya Mambo ya Nje ambapo pia waliibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya mchezo  kumalizika bila kufungana
  Nahodha wa timu ya Kamati ya Amani Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum, akimiliki mpira mbele ya beko wa VPO Sports Club,Bakari Kibiti wakati wa Bonanza maalum la kumuaga Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, lililofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete,uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam  jana Nov 28, 2015. Katika Mchezo huo VPO walishinda kwa bao 1-0 na kutinga fainali na Timu ya Mambo ya Nje ambapo pia waliibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya mchezo  kumalizika bila kufungana.
 Mchezaji wa  VPO Sports Club, Nehemia Mandia, akimtoka beki wa timu ya Kamati ya Amani, Mhungaji Amos Nene, wakati wa Bonanza maalum la kumuaga Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, lililofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete,uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam  jana Nov 28, 2015. Katika Mchezo huo VPO walishinda kwa bao 1-0 na kutinga fainali na Timu ya Mambo ya Nje ambapo pia waliibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya mchezo  kumalizika bila kufungana.
 Dkt. Bilal akisalimiana na wachezaji wa Kamati ya Amani kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
 Dkt. Bilal akisalimiana na wachezaji wa Timu ya VPO Sports Club labla ya kuanza kwa mchezo huo.
Dkt. Bilal akisalimiana na wachezaji wa Timu ya VPO Sports Club labla ya kuanza kwa mchezo huo.
 Mchezaji wa Amana Bank akimjaribu kumiliki mpira huku akizongwa na beki wa Mambo ya Nje. Katika mchezo huo Mambo ya Nje walishinda mabao 2-1
 Mgeni rasmi akifuatilia mchezo uliokuwa ukiendelea uwanjani hapo
 Dkt. Bilal akisalimiana na wachezaji wa Timu ya VPO Sports Club labla ya kuanza kwa mchezo huo.
 Dkt. Bilal akisalimiana na wachezaji wa Timu ya VPO Sports Club labla ya kuanza kwa mchezo huo.
Dkt. Bilal akisalimiana na wachezaji wa Timu ya VPO Sports Club labla ya kuanza kwa mchezo huo.
**********************************
Na Muhidin Sufiani, Dar
Timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, imetwaa kombe la bonanza maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kumuaga rasmi Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kwa kuifunga kwa mikwaju ya penati 5-4 timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika mchezo wa fainali.
Katika bonanza hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Park (JMK Park) zamani Kidongo Chekundu, timu hiyo iliianza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kamati ya Amani Tanzania iliyoongozwa na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum.
Baada ya mechi hiyo, Timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais ilicheza mchezo wa fainali dhidi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambayo ilimaliza katika nafasi ya pili, ilifuzu katika hatua hiyo baada ya kuifunga timu ya Amana Benki kwa mabao 2-1.
Katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu, timu ya Amana Benki iliifunga timu ya Kamati ya Amani kwa mabao 2-0. Makamu Rais Mstaafu Dk Bilal alishuhudia michezo yote hiyo na kukabidhi vikombe kwa washindi.
Akizugumza baada ya michezo hiyo, Dkt. Bilal, aliwashukuru waandaaji wa bonanza hilo kwa kumuaga rasmi na kusema michezo ina umuhimu mkubwa sana katika maisha ya kila siku ya binadamu ikiwa ni pamoja na kujenga afya, kuhimarisha na kuanzisha urafiki na vile vile kuburudisha.

“Nimefurahi sana kuona jinsi mlivyoonyesha ushindani mkubwa na vipaji vya hali ya juu, sikujua kama kuna wachezaji wazuri namna hii, nawapa pongezi sana na msiache kuandaa mabonanza mengine kama haya mara kwa mara, mnatakiwa kufanya kila mara ili kujenga afya zenu na kuanzisha na kudumisha urafiki na amani” alisema Dkt Bilal.
Aidha Dkt.  Bilal alitoa wito kwa wanamichezo nchini kutumia uwekezaji huo mkubwa kutoka kwa Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete kuendeleza vipaji. “Hapa kuna viwanja vya mpira wa miguu, mpira wa kikapu,  netiboli, mpira wa mikono, mpira wa wavu, tumieni fursa hii kwa ajili ya kuendeleza vipaji na kuiwezesha nchi kufanya vyema katika michuano ya Kimataifa,” alisema.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa