Na Beatrice Lyimo- MAELEZO
09/05/2016
DAR ES SALAAM.
Serikali
imewataka wananchi wasio na uwezo wa kuweka Mawakili au kulipa huduma
za kisheria kutumia Mpango wa Huduma za Msaada wa Kisheria kupitia
Sekretarieti ya Msaada wa Kisheria na Mashirika yaliyosajiliwa kwa ajili
hiyo.
Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizaraya Katiba na Sheria Bi.
Sheiba Bulu alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu huduma
hiyo inayotolewa na Sekretarieti ya Msaada wa Kisheria na Mashirika
yaliyosajiliwa kwa ajili hiyo.
Amesema
kuwa lengo kuu la huduma hiyo ni kuhahikisha kila mwananchi anapata
haki katika mamlaka husika za utoaji haki na kwa wakati.
“Sekretarieti
ya Msaada wa Kisheria inatoa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi
ambao ni wahitaji wa msaada wa huduma za kisheria na kuwapa ushauri juu
ya masuala mbalimbali yanayowakabili,” aliongeza Bi. Sheiba.
Aidha,
kwa upande wake Wakili wa Serikali Mkuu kutoka Wizara hiyo, Charles
Mmbando amezitaka asasi na mashirika yanayojishughulisha na huduma ya
msaada wa kisheria kwa wananchi kujitangaza ili kuzidi kutambulika katika jamii kwani wizara yake inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na mashirika hayo.
Mpango
huo ulianzishwa mwaka 2012 ili kuwezesha asasi na Mashirika yasiyokuwa
ya kiserikali kupanua wigo wa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi
waishio kwenye maeneo ambayo hawawezi kulipia gharama za mawakili
nchini.
0 comments:
Post a Comment