WAKALA
ya Mkemia Mkuu wa Serikali imekusudia kuendesha kampeni maalum ya
kupima matumizi ya vilevi kwa madereva wanaosafirisha abiria na mizigo
ikiwa ni hatua ya kukabiliana na tatizo la ajali za barabarani nchini.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali Prof.
Samwel Manyele alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wadau wa
kemikali juu ya matumizi salama ya kemikali nchini.
Prof.
Manyele alisema utaratibu wa kuwapima madereva hao utaanza hivi
karibuni na utawezesha kupunguza tatizo la ajali barabarani na kuvitaka
vyombo vya ulinzi na usalama kutoa ushirikiano katika zoezi hilo.
“Madereva wote wanaosafirisha mizigo na abiria watatakiwa
kupita kwenye kipimo ambacho kitaonyesha kama madereva hao wanatumia
vilevi, hali hiyo itasaidia kutatua tatizo la ajali za barabarani
nchini”, amesema Prof. Manyele.
Aidha, Prof Manyele alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kutoa uwezo na uelewa kwa wahusika hasa wasimamizi wa shughuli za kemikali na matumizi salama juu ya kukabiliana na matukio au ajali za kemikali pale yanapotokea.
Aliongeza
kuwa mafunzo hayo yamekuja kufuatia uelewa mdogo wa elimu kwa baadhi ya
wadau wanaojishughulisha na masuala ya kemikali kuhusu uzalishaji,
uhifadhi, usimamizi na usafirishaji wa matumizi ya kemikali nchini.
Mbali
na hayo, Prof Manyele alisema kumekuwa na ajali na matukio yanayotokana
na kemikali ikiwemo ya ajali halisi na mengine kutokana na kukosa
uelewa wa matumizi sahihi na salama ya kemikali.
Akifafanua
zaidi Prof. Manyele alisema katika kukabiliana na madhara yatokanayo na
matumizi yasiyo salama ya kemikali, Serikali ilitunga sheria ya
Kemikali za Viwandani na majumbani mwaka 2003 kwa lengo la kuhakikisha
kemikali hizo zinatumika katika hali iliyo salama.
0 comments:
Post a Comment