Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Mamlaka
ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imejizatiti kurudisha thamani ya
huduma za bima kwa kubadilisha baadhi ya sheria na kanuni za bima pamoja na kutengeneza mfumo wenye kutoa tija kwa Wananchi, Serikali pamoja na Kampuni za Bima nchini.
Hayo
yamesemwa na Kamishna wa Bima, Baghayo Saqware alipokuwa akiongea na
waandishi wa habari juu ya namna mamlaka hiyo ilivyojipanga kurudisha
thamani ya bima kwa wananchi na makampuni ya bima hapa nchini, leo
Jijini Dar es Salaam.
Baghayo
Saqware amesema kwamba moja ya kanuni na sheria zitakazoboreshwa ni
pamoja na kupeleka biashara ya bima (Insurance business – risks) nje ya
nchi badala ya kutumia makampuni ya ndani.
“Tutaweka kanuni itakayolazimisha Kampuni za bima hapa nchini kuongeza mitaji
au kutengeneza mfuko wa pamoja au mfumo wa makampuni kushirikina
kimtaji ili kuweza kuandikisha na kubakisha sehemu kubwa au biashara
yote ya bima nchini,” alifafanua Saqware.
Aliendelea
kwa kusema kuwa utawekwa utaratibu wa kisheria utakaohakikisha
waingizaji wa mizigo kutoka nje ya nchi wanakatia bima za mizigo yao
kupitia kampuni za bima nchini.
Aidha
amesema kwamba ikibidi mamlaka hiyo itabadilisha sheria ya bima nchini
ili wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa kutoka nje ya nchi (import goods) iwe ni lazima kukatia bima nchini ili kuongeza mapato ya kodi (VAT) pamoja na bima (Premium Levy).
Katika
kurudisha thamani ya huduma ya bima kwa wananchi mamlaka hiyo
itahakikisha makampuni yanayotoa huduma ya bima yanatoa huduma stahiki kwa wateja wa bima pamoja na kuhakikish malalamiko ya wateja yanayofikishwa katika mamlaka husika yanashughulikiwa kwa wakati.
Aidha,
katika kupanua shughuli za bima mamlaka hiyo iko katika hatua za mwisho
za kukamilisha bima ya kilimo, mifugo pamoja na bima za watu wenye
kipato cha chini (Micro-insurance) pamoja na kukamilisha utekelezaji wa
sera ya Taifa ya Bima.
Vile vile inapanua matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) kwa kutumia utaratibu wa kusajili na
kutoa leseni za biashara ndani ya siku saba hadi thelathini, aidha
mfumo huo utaondoa tatizo la bima bandia za vyombo vya moto pamoja na
kuhakiki uhalali wa stika za bima kwa walionazo.
Nae, Meneja Tehama TIRA, Aron Mlaki amesema kwamba mfumo huo wa Tehama utamuwezesha mwananchi kupata maelezo ya bima yake kupitia intanenti na meseji za kawaida ambapo kwa upande wa message za kawaida ataandika neno ‘STIKA’ likifuatiwa na namba ya Stika na kuituma kwenye namba 15200 baada ya hapo atapokea taarifa za bima yake.
0 comments:
Post a Comment