Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » ASKARI KORTINI KWA MAUAJI

ASKARI KORTINI KWA MAUAJI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Imeandikwa na Mohammed MussaASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Marwa Wambura (25) amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya hakimu mkazi Kinondoni kwa tuhuma za kuua.
Akisomewa mashitaka hayo kwa mara ya kwanza katika Mahakama hiyo, mbele ya hakimu Isic Kuppa, mwendesha mashitaka Joseph Nasua alidai kuwa Juni 17, 2017, maeneo ya Kibamba CCM, wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, mtuhumiwa Rashid Sadick alitenda kosa hilo huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza shitaka hilo.
CHANZO HABARI LEO
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa