Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa Habari
kuhusu kambi maalum ya matibabu ya Moyo inayofanywa na Taasisi hiyo kwa
kushirikiana na Taasisi ya Madaktari Afrika ya nchini Marekani kwa
wagonjwa ambao mapigo yao ya moyo yako chini sana na hivyo kuwekewa
kifaa maalum cha kurekebisha mapigo ili yawe sawa (kwa jina la kitaalamu
Pacemaker) . Kushoto ni Daktari Bingwa na Magonjwa ya Moyo Mathew
Sackett. Tangu kuanza kwa kambi hiyo mwanzoni wa juma hili jumla ya
wagonjwa 20 wameshapatiwa matibabu kati ya hao nane wamewekewa Pacemaker
na wengine wanne wanatarajia kuwekewa leo na kesho.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akiwaonyesha waandishi wa Habari
jina la Dkt. Mathew Sackett wa Taasisi ya Madaktari Afrika ya Nchini
Marekani lilivyoandika katika nguo yake wakati wa mkutano baina yao
uliozungumzia kambi maalum ya matibabu ya Moyo inayoendelea katika
Taasisi hiyo kwa wagonjwa ambao mapigo yao ya moyo yako chini sana na
hivyo kuwekewa kifaa maalum cha kuyarekebisha ili yawe sawa (kwa jina la
kitaalamu Pacemaker) .
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tulizo Shemu na mwenzake kutoka Taasisi ya
Madaktari Afrika ya Nchini Marekani Mathew Sackett wakimwekea mgonjwa
kifaa maalum cha kurekebisha mapigo ya moyo ili yawe sawa (kwa jina la
kitaalamu Pacemaker) kifaa hicho huwekewa wagonjwa ambao mapigo yao ya
moyo yako chini sana. Tangu kuanza kwa kambi maalum ya matibabu ya moyo
jumla ya wagonjwa nane wameshawekewa Pacemaker na wengine wanne
wanatarajia kuwekewa leo na kesho.
Wataalamu wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) na wenzao wa Taasisi ya Madaktari Afrika ya Nchini
Marekani wakimwekea mgonjwa kifaa maalum cha kurekebisha mapigo ya moyo
ili yawe sawa (kwa jina lakitaalamu Pacemaker) kifaa hicho huwekewa wagonjwa ambao mapigo yao ya moyo yako chini sana.
0 comments:
Post a Comment