Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi
wa Wilaya ya Kinondoni (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi
katika wilaya ya kinondoni
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa
Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Kairuki amesema uhakiki wa kina utasaidia sana kuepukana na kutojirudia tena kwa
suala la watumishi wa umma wanaoghushi vyeti.
“Jana tumetoa vibali vya ajira 10,184 kwa
Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Wakala za Serikali, pamoja
na Taasisi na Mashirika ya Umma ili kujaza nafasi zilizoachwa na watumishi wa
umma waliobainika kughushi vyeti vya elimu, hivyo napenda niwasisitize sana waajiri
wote kufanya uhakiki wa kina ili tusiwe tena na watumishi wa umma wasiostahili
katika orodha ya malipo” Mhe. Kairuki amesema.
Waziri
Kairuki amesisitiza kuwa zoezi la uhakiki ni endelevu ambapo lazima lifanyika
pale mtumishi wa umma atakaporudi katika kituo cha kazi kutoka masomoni, na watakaorejea
katika utumishi wa umma baada ya likizo
bila malipo au sababu nyingine.
“Tunafanya
hivi sio kwa nia mbaya, bali tunataka tuwe na watumishi wanaostahili kuwepo
katika utumishi wa umma kwa sababu wanaoghushi wanaziba nafasi za wale
wanaostahili kuwepo na wenye sifa katika utumishi wa umma” Mhe. Kairuki
aliongeza
Pia
amewataka Waajiri kusafisha taarifa wa watumishi wa umma mara kwa mara katika
Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS).
“Kuna
watumishi ambao muda wao wa kuwepo kazini umemalizika (wamestaafu) lakini bado
wanaendelea kuwepo, Mfumo wa HCMIS sasa kila ifikapo saa 06:01 usiku utakuwa unawaondoa
wale wote ambao muda wao wa kuwepo kazini umefika lakini bado wanaendelea
kuwepo kwenye Mfumo.
Mhe,
Kairuki yuko katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es Salaam, ambapo leo ni
siku yake ya nne aliyoitumia kukutana na Watendaji na watumishi wa umma wa Halmashauri
ya Manispaa ya Kinondoni, baada ya
kuzungumza na watumishi wa umma wa Temeke na Mbagala.
Lengo
la ziara ni kukutana na watumishi wa umma na kusikiliza malalamiko, ushauri na
changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kuzifanyia kazi
na kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma nchini.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi
ya Rais-UTUMISHI
0 comments:
Post a Comment