MRADI mkubwa wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), uliopo Kawe Dar es
Salaam ambao ulisimama kwa mwaka mmoja kutokana na sababu mbalimbali,
umeanza kazi na kwamba unalenga kufanya eneo hilo kuwa Kitovu cha
Biashara jijini humo.
Akizungumza wakati wa ziara iliyofanywa na Kamati ya Mipango miji na
Mazingira Manispaa ya Kinondoni, Mkurugenzi wa NHC, Nehemiah Mchechu,
alisema mradi huo unatarajiwa kukamilika kati ya mwaka 2019 na 2020
ambao unagharimu zaidi ya dola za kimarekani bilioni mbili.
Mchechu alisema sababu za kusimama kwa mradi huo walikuwa wanasubiri
kujiridhisha namna ya uendeshaji wa mradi huo ikiwemo gharama zote
pamoja na kupata kibali kutoka Wizara ya Fedha.
“Mradi huu unaojulikana kama 711, utawanufaisha watu zaidi ya 50,000
kwa kuwa utakuwa na biashara kwa saa 20,’’ alisema. Pia alisema
wanategemea mradi huo utaleta maendeleo kwa miaka 50 ijayo kwa kuwa
licha ya kuwepo kwa makazi 262, watajenga miundombinu ya usafiri.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment