Imeandikwa na Mwandishi Wetu
SERIKALI imetoa onyo kwa watumishi wa umma wanaotoa siri za serikali
na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii kuwa watachukuliwa hatua za
kisheria.
Onyo hilo lilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Waziri wa Ofisi ya
Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki (pichani) wakati
wa ufunguzi wa mkutano wa watumishi wa umma wa Manispaa ya Ubungo.
Kairuki alisema mtumishi wa umma atayejihusisha na usambazaji wa
taarifa za serikali, atachukuliwa hatua za kisheria ikiwamo kufikishwa
mahakamani na kupewa kifungo cha miaka 20 jela. Alisema serikali ina
utaratibu wake wa kutoa taarifa kwa umma ikiwa ni pamoja na kupitia
machapisho yake kwa jamii
CHANZO HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment