Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » MIILI INAYOOKOTWA BADO KUTAMBULIWA-IGP

MIILI INAYOOKOTWA BADO KUTAMBULIWA-IGP

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Imeandikwa na Lucy Lyatuu
IGP Simon Sirro.
JESHI la polisi nchini limesema hadi sasa hakuna watu waliojitokeza kutambua au kulalamika kwamba wamepoteza ndugu zao kufuatia kuwapo kwa idadi kubwa ya miili inayookotwa maeneo mbalimbali.
Miili hiyo imekuwa ikiokota ikiwa imewekwa kwenye viroba na mingine ikiwa imefungwa mawe makubwa na kamba. Mkuu wa Jeshi hilo nchini (IGP), Simon Sirro alisema kumekuwepo na changamoto ya kuwapata watu wanaodai kupotelewa na ndugu zao, ili Polisi waweze kufuatilia kwa karibu kadhia hiyo.
Alisema Jeshi hilo lilitoa taarifa za kuokotwa kwa miili hiyo katika maeneo mbalimbali, hususani katika jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya upelelezi wa vinasaba (DNA) lakini hawajaona mtu yeyote aliyejitokeza kwa ajili ya kutambua mwili wowote ule.
Sirro alisema kutokana na hali hiyo, jeshi hilo linaendelea kupeleleza na baada ya hapo utaratibu mwingine uweze kufuatwa. “Kimsingi bado hakuna mwili hata mmoja uliotambuliwa wala ambaye amefika kutambua, hivyo utaratibu mwingine unaendelea kwa aliyeshindwa.
CHANZO HABARI LEO 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa