SIKU chache baada ya Lazaro Nyalandu kutangaza kujiuzulu nafasi zake
zote ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Ubunge wa Singida
Kaskazini, Tume ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa haina taarifa kuhusu
mbunge huyo na kwamba watakapoipata watatoa utaratibu unaopaswa
kuchukuliwa.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhani Kailima alisema hayo jana
mchana, ikiwa ni siku moja baada ya Ofisi ya Spika Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kutoa taarifa kuwa wameshawasilisha barua kwa
mkurugenzi huyo kumtaarifu shauri la Nyalandu la kupoteza sifa za kuwa
mbunge.
Kailima alisema, “Mpaka sasa hatujapata taarifa yoyote kuhusu
mheshimiwa Nyalandu, kama taarifa hiyo itafika kwetu tutatoa taarifa kwa
umma”. Akitoa ufafanuzi kuhusu sheria zinazopaswa kufuata, alisema kuwa
Ubunge unaweza kukwama pale mbunge au mbunge wa viti maalumu
atakapovuliwa uanachama na chama cha siasa, au kuamua kuachana na chama
CHANZO HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment