Home » » TSN WAKUMBUSHWA WELEDI KATIKA KUHABARISHA

TSN WAKUMBUSHWA WELEDI KATIKA KUHABARISHA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Imeandikwa na Matern Kayera
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Susan Mlawi akizungumza na wakuu wa Idara za Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) alipofanya ziara kwenye makao makuu ya ofisi hizo, Dar es Salaam jana. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Nicolas William, Mhariri Mtendaji wa TSN, Dk Jim Yonazi (kulia kwake), Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi. (Picha na Fadhili Akida).
TSN wakumbushwa weledi katika kuhabarisha fursa ya soko kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na ndiyo maana imeanza kuyapeleka magazeti ya HabariLeo na Daily News kwenye baadhi ya nchi hizo ikiwemo Kenya na Rwanda, lakini lengo ni kuyapeleka kwenye nchi zote wanachama wa Jumuiya hiyo pamoja na Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Dk Yonazi alisema TSN pia inachapisha majarida mbalimbali, mabango, vitabu, kalenda, madaftari, ripoti na machapisho mengine pamoja na kutengeneza makala ya televisheni mbalimbali kama vile mambo ya afya, maliasili, utalii, lakini pia alisema TSN iko tayari kutengeneza makala ya televisheni kwa ajili ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ifikapo mwaka 2019.
“Pia bidhaa yetu nyingine tuliyoianzisha mwaka huu ni Jukwaa la Biashara. Jukwaa hili linatusaidia katika masoko, kuitangaza mikoa na kuibua fursa mbalimbali zilizopo kwenye mikoa hiyo na hivyo kuwasaidia wananchi na wadau wengine kuzijua fursa hizo.
Tulianzia mkoani Simiyu na sasa tutaenda mikoa ya Geita, Dar es Salaam na Zanzibar, lakini pia tutatengeneza jukwaa maalumu la biashara la wanawake na tutazindua ‘magazine’ya wanawake mkoani Dodoma,” alisema Dk Yonazi.
Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Mlawi aliongozana na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Nicholaus William pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Habari -Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi.
CHANZO HABARI LEO

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa